Monday, December 29, 2008

THE MOST EXPENSUVE PLAYER IN BONGO



Kati ya wachezaji wakibongo ambao wataukumbuka mwaka 2008 ni Juna K. Juma. Alinunuliwa kutoka Simba kwenda Yanga kwa gharama ya shilingi millioni 40 za kitanzania, akiwa analipwa mshahara mnono na malupulupu kibao japo hakichezea timu ya taifa Taifa Stars.

RAC MWAKA 2008 MMMMMHHHH!!!



Alijaribu sana lakini hakupatya mafanikio yanayoendana na jina lake kwa mwaka 2008. Lakini alisikika sana kwenye vyombo vya habari kutokana nna mahusiano yake na mwana hip hop wa Arusha Lody Eyes. Je mwaka 2009 atafanya nini kurejesha heshima yake

AMEBAMBA SANA MWAKA 2008



Mwaka 2008 ulikuwa mwaka wake hasa kwa upande wa hip hop, wimbo wake wa Lolipop umeuza na umejulikana kila pembe ya dunia. Kama hiyo haitosho albam yake ya THE CARTER 3 nayo imeharibu vibaya mno kwenye mauzo ana mbaya ambayo kwake ni nzuri zaidi ni kufunika kwenye kolabo za wasanii wenzake

ULISHAWAHI KUUONA MZIGO HUU!!!!



Hii ni moja kati ya picha za utani ambazo zilisambaa sana mwaka 2008 ikimwonyesha George Bush akiwa katika pozi la furaha na marehemu Saadam Hussein aliyekuwa rais wa Iraq.

JOHN CENA AFUTIWA MASHITAKA



Crew ya muziki ya nchini Marekani inayojulikana kwa jina la M.O.P (Mashout Posse) wamefuta kesi waliyokuwa wameifungua maalum kwaajili ya nyoyta wa mieleka wa WWE John Cena kuwa alichukua vikorombwezo kutoka kwenye wimbo wao na kuutumia kwenye wimbo wake anaoutumia kuingilia kwenye ulingo pindi anapokuwa kwenye mashindano ya mieleka.
Hasijajulikana kwanini kundi hilo limeamua kuyafuta mashitaka hayo, kwaiyo kwa sasa Cena ambaye ni kipenzi cha wengi ataendelea kuutuia wimbo huo.

Saturday, December 27, 2008

NAWATAKIA MWAKA MPYA MWEMA

HAPPY NEW YEAR



Nashukuruni sana wadau na watu wote tuliokuwa pamoja kwa mwaka mzima wa 2008 na sasa Mungu anatujalia ndio hivyo tena tunauaga mwaka huu na kuukaribisha mwaka 2009. Wale wote mliokuwa mkinitumia mails nasema THANX A LOT WATU WANGU NAWAPENDA WOTE.
Amani iendelee kutawala ila ushauri wangu ni kuwa mwaka unaisha kaa chini fikiria umefanya kitu gani cha maana mwaka 2008 ambcho unaweza ukajivunia hata mbele za watu, ili iwe challange kwa mwaka unaofatia.

Kwa mawazo, ushauri na chochoote unachotaka kushare nami nicheki kupitia haramba29@yahoo.co.uk

CHEMSHA BONGO WIMBO BORA



Mkongwe wa kwenye game la muziki wa kizazi kipya JOSEPH HAULE wimbo wake wa "Chemsha Bongo" alioufanya enzi zile yupo na kundi la HBC umechaguliwa kuwa wimbo bora kwa miaka kumi ya kituo cha radio cha Clouds FM tangu kilipoanzishwa mpaka leo.
Clouds alicheza nyimbo 50 bora tangu kuanzishwa kwa radio hiyo miaka 10 iliyopita, baada ya ushindi huo Jay akiwa na BIG WILLE mmoja kati ya memba waliokuwa wakiunda kundi hilo wameahidi kuwa wanakuja tena upya na alba ya kundi soon

Monday, December 22, 2008

T-PAIN

BEEF vs T-PAIN



Ebwana hee washaji zangu hasa nyinyi wapenda hip hop inasemekana kuna kabeef kachinichini kanaibuka kati ya Plies na T-Pain, ni kuhusu nini na imekuaje ngoja ni brows kisha nitawajulisheni wana au vipibaaab>>>>

MAN UTD OYEEEEEEEE



Club ya Man Utd imetwaa ubingwa wa dunia wa vilabu huko katika jiji la wajapani baada ya kuifunga timu ya LDC ya Ecuador kwa goli moja kwa bila, shukrani kwa Rooney aka Mr Maubavu aliyeingiza kimiani koli hilo dk ya 73.

JANET BADO HAJAPATA KITUMBO



Kufuatima maneno mengi kusemwa juu ya hali ya dada wa Michael Jackson, hapa namzungumzia Janet kuwa ni mjamzito. Boyfriend wa mwanamuziki huyo JD amekana habari hizo na kusema kuwa Mrs wake huyo to be hana ujauzito. Maneno hayo yalizuka wiki kadhaa zilizopita kutokana na Janet kukatisha ziara zake za kimuziki alizokuwa akizifanya.

BECKHAM ATUA AC MILAN




Baada ya kukilmbilia Marekani anakocheza mpaka sasa katika timu ya LA GALAX mchezajia ambaye yupo kibiashara zaidi David Beckham aimaye ametua rasmi katika club yaAC Milan kwa mkopo wa miezi mitatu, japo kiungo wa timu hiyo Gattuso ambye kwa sasa ni majeruhi amenukuliwa akimponda kimtindo mchezaji huyo kufuatia ujio wake wa miezi mitatu katika timu hiyo kuwa ni sawa na bure.

Tuesday, December 16, 2008

MODO STEJINI



Prisca Sulle, mmoja kati ya wasaichana wanaofanya vizuri katika medani ya u-modo TZ akiwa anapita stejini katika moja kati ya kazi zake za kila mwisho wa wiki.

POZI ZA KICHOKOZI



Rihanna akiwa na Chriss Brown stejini wakiwa wanapafom pamoja wiki hii huko Marekani.

CLUB LEMAMBO YA WAJANJA




Kwa wale wajanja wote wa town msikose kujimix ndani ya CLUM LEMAMBO iliyopo mitaa ya Ubungo-External. Chini ya DJZ wakali kama vile DJ KIPASO , DJ DENIS bila kumsahau DR K.
CHEK RATIBA YAO
IJUMAA NA JUMAMOSI: Disco la nguvu na mixing za kijanja kutoka kwa DJz
JUMAPILI: Kutakuwa na muziki wa nguvu na vitu flani mixer ma-surprise kibao ambapo itakuwa inaishia mida ya saa saba usiku ili kuwaruhusu watu wajiandane na kazi siku inayofatia.
Mmoja kati ya waandaaji wa inshu hiyo amenidokeza kuwa “Kuna vitu kibao vinakuja maalum kwaajili ya watu wetu, waendelee kuview muzikimnene watajua maujanja yote mwana” alisema Dr K.

50 KUTOMWACHA SLIM SHADDY


Licha ya kwamba albam yake ijayo itakayo julikana kwa jina la “Before I Self Destruct” kutoka kwa 50 Cent ndio itakuwa ya mwisho akiwa chini ya mkataba wa Shady/Aftermath inayomilikiwa na rapa Eminem, msanii 50 Cent amesema kuwa kamwe hato mwacha mshkaji wake huyo yaani Eminem na wataendelea kuwa marafiki wa karibu licha ya kuwa hatokuwa chini yake tena.

VIBAKA NAO HAWAKUCHEZA MBALI




Hapa lilitokea sekeseke moja baada ya jamaa mmoja kutaka kumpora mwenzake si ndipo akashtukiwa, du kilichofuata ni ........

MAXIMO AKITOA HI KWA FANS



Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars akipewa mikono ya pongezi kutoka kwa mashabiki waliokuwa wamefika uwanjani hapo kuwapokea mashujaa.

JAMANI USHINDI RAHA NYIE WE ACHA TU




Yaani ilikuwa ni full kujiachia mwanangu kama ulikosa msafara huu na wewe upo Dar basi utaendelea kujilaumu kwa kukosa tukio hili la kiistoria katika maisha ya kizazi cha sasa kwa sisi wa Bongo.

NYOMI LILIKUWA SI LA KITOTO



Undahani na mimi mwanawane nitabaki nyuma wakati pande za Airport ndio moja kati ya maskani yangu nilijichanganya kwa sana tu sema nilikosa mtu wa kunifotoa na mimi ikabidi niwe mpole nikiwafotoa wenzangu huku roho ikinima kwa saaaana.

MAPOKEZI YA STARS



Ilikuwa ni full kujiachia kama unavyowacheki wabongo waliouwa pamoja na vijana wa ACUDO IMPACK wakihiachia kwa kusheerekea ushindi dhidi ya Sudan

Monday, December 15, 2008

UZINDUZI WA ZERO K @ FREETIME RESORT




Kama kawa wanabongo flava wanazidi kujiachia ndani ya muzikimnene.blogspot.com Ijumaa hii nazungumzia tarehe 19 -12-2008 kijana anayekuja kwa kasi kwenye game ya kibongo akiwa anajulikana kwa jina la ZERO Kanatarajia kuzindua albam yake inayojulikana kwa jina la KUR hilo jina, hilo ni jina la moja kati ya track zilizomo humo ndani. Badhi ya singos JAAN.
Mshakaji sio kwamba ni mwarabu usishangae kwaalizozirelease ni “Njoo Basi” na “Sinyorita”.
Mshkaji anapata sapoti kubwa sana kutoka kwa vijana wa Uhuru FM, WAKALI DJZ. Pichani ni mmoja kati ya memba wa wakali DJZ, Dr K alipokuwa akilonga name.

Pichani ni mmoja kati ya memba wa WAKALI DJZ from UHURU FM akijulikana kwa jina la DR K.

TENGA OYEEEEE




Aliyekuwa Rais wa TFF chini Tanzania jana alikabidhiwa madaraka ya kuendelea na cheo chake hicho kwa muda wa mika minne ijayo baada ya kumwaga aliyekuwa mpinzani wake Jamal Malinz,
Hongera Tenga sasa endeleza makamuzi ya ukweli au sio FAZA????

ETI AKA NDIO KAJAMAA NDIO KA MUZIKIMNENE???




Wajameni hee kuna wadau wangu walikuwa wananiambia eti mimi sura yangu kama paka ndio maana sipendi kujiuzisha kwenye blog yangu,,jamani siyo kiivyo hata mimi ni ka-handsome kadogodogo we mwenyewe si unanichek au kweli nafanana na mbwa au paka.

You know wat??? i go by ze name JOHN JOSEPH HARAMBA

NIAJE FANS WA MUZIKIMNENE



Jamaa anajulikana kwa jina la Sama Misago ni mtangazaji wa MAGIC FM, hapa akiwa anakamua ndani ya studio. Alikutana na dogo wa muzikimnene na wakapiga story mbili tatu. Thanx kwa sapoti yako ndani ya MUZIKIMNENE....MUCHI LOVE BRO!!

NI Z-ANTO TENA!!!




Hivi karibuni baada ya ukimya wa muda mrefu tangu alipokuwa akitamba na ngoma yake ya "Binti Kiziwi" hatimaye Z-Anto amerejea tena kwenye game kwa kuachia track inayojulikana kwa jina la "Peace & Love" humo ndani akiwa amewapa mashavu memba mwenzie wa TIP TOP CONNECTION namzungumzia Pingu pamoja na mkali kutoka pande za Kenya Jua Kali.
Je wadau wanasubiri hile ilikuwa kabahatisha au kweli mshkaji mkali, tusubiri na tuone ngoma hiyo itapokelewa vipi?

MISS WORLD AKITABASAMU

MISS TZ CHALI KAMA KAWA



Hatimaye mrebo wetu Nasreen Kaim ametoka kappa katika shindano la Miss World lililofanyika jumamosi iliyopita huko Johannesburg, South Africa ambapo mshindi wa shindano hilo amekuwa ni mrembo kutoka Russia ambaye katika kujibu swali alipokuwa kwenye hatua ya watabo bora ilibidi atafsiliwe na mkalimani wake kutoka lugha ya kiingereza kwenda kirusi nandipo alipoweza kujibu swali aliloulizwa.
Pole sana mrembo wetu, hakuna cha kufanya rudi tu bongo kwa Mh Rundenga ajipange upya tusubiri tena zali kama la Nansy Sumari miaka 20 ijayo.
LAKINI WADAU WANGU EHEE HIVI VIPI MBONGO ANGEINGIA KWENYE TANO BORA HALAFU AKAOMBA ATAFSILIWE SWALI KWA KISWAHILI, MMMMHHH SIPATI PICHA MANENO YA WABONGO HAPO….

OYE OYE TAIFA STARS




Baada ya miaka 28 Taifa Stars imefanikiwa kuwakilisha tena kwa kufanikiwa kuidunga Sudan jumla ya magoli 5-2 nakufanikiwa kutita kwenda kucheza kwenye mashindano ya Afrika yanayohusisha wachezaji wa ligi za ndani za Afrika pekee zitakazofanyika mwezi wa saba mwakani huko Ivory Coast.
Mara ya mwisho kwa timu ya taifa ya Tanzania kucheza mizhuano ya Afrika ilikuwa mwaka 1980 huko Lagos, Nigeria (Du hii ni kali hata mimi John nilikuwa sijazaliwa).
Katika mechi ya kwanza Stars ilishinda 3-1 na mechi ya marudianao iliyofanyika Sudani Stars imeshinda 2-1. Kwa niaba ya washkaji zangu wanaonisababisha mimi nikaweza kuwaletea haya maujanja ya MUZIKIMENENE ,,naipongeza Taifa Stars na wote waliosababisha ushindi huo

Saturday, December 13, 2008

Friday, December 12, 2008

CHRISS BROWN APANDA CHATI



Kwa muzjibu wa BILLBORD dogo aliyekimbiza vya kutosha mwaka huu CHRISS BROWN amechaguliwa kuwa msanii bora wa mwaka yaani BEST ARTISTE THE YEAR

SAADAT ANARUDI TENA




Hivi unamkubuka huyu jamaa??? kama utakuwa ni mfuatiliaji kiasi wa muziki wa BONGO FLAVA utakuwa unamkumbuka, Jamaa anaitwa SAADAT aliwahi kutamba sana kupitia wimbo wake wa "Haiwezekani" aliokuwa kamshirikisha Mr BLU, wimbo ambao ulitengenezwa kwenye studio ya G Records.

Hivi sasa anasema anatarajia kurejea na ujio mpya kwenye game lakini this time anakuja sio msanii wa kurap pekee bali pia atakuwa anaimba kama unavyomchek akiwa kakamatilia gitaa akimwonyesha JOHN wa muzikimnene jinsi alivyofit kwenye gitaa.

Haya bwana sisi tunangojea ageuke,,aahh ahh No tunangoja ujio wako mpya kaka.

Thursday, December 11, 2008

PRISCA STEJINI




Umri wake ni mdogo lakini mambo yake kwenye modeling industry ni makubwa, anajulika kwa jina la Prisca Sulle mwanamitindo mwenye umri wa miaka 23. Kwa sasa ameshatuma maombi kwa mawakala wa nje anachosubilia ni majibu tu ili aweze kwenda nje ya Bongo kutuwakilisha levo zile za kimataifa. alisema hayo alipokuwa akizungumza na JOHN wa muzikimnene

TID YUPO HURU




Msanii Khalid Mohamed ameachiwa huru kutoka jela kutokana na msamaha wa rais Jakaya Kikwete, msanii huyo anayejulikana sana kwa jina la TID alikuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kutokana na kupatikana na kosa la kumshambulia kwa kumpika mmkazi mmoja wa jijini Dar kwenye ukumbi wa Slipway.

Msamaha huo umekuja siku ambayo Tanzania (wakati ule Tanganyika) ikisheherekewa kutimiza miaka 47 tangu ipate uhuru wake kutoka kwa wakoloni.

WANA KWAYA KAZINI




Wanakwaya wakiwa wanafanya shooting ya moja kati ya nyimbo zao katika viwanja vya Mwalim Nyerere International Airport kama walivyokutwa na John wa muzikimnene. Kwaya hii inapatikana maeneo ya Banana Dar es salaam

HAPA NI KAZI TU




Hii ngoma haina kuremba, vijana wanaojishuhulisha na ubebaji wa taka katika maeneo mbalimbali wakiwa mzigoni maeneo ya Kipawa jijini Dar es salaam.

MR KISS KISS & RIHANNA




Wasanii chipukizi ambao wanabamba kwenye anga za muziki wa r&b ambao inadaiwa kuwa wanamahusiano ya kimapenzi licha ya wao kuwa wanakana na kudai kuwa ni marafiki, picha hii imetumika as a front cover ya kwenye magazine ya VIBE, inayoonyesha wakiwa pamoja.

Tuesday, December 9, 2008

BINAMU @ CINE CLUB




Hii ilikuwa before party uliyofanyika CINE CLUB ambapo wasanii MWANAFALSAFA akiwa na AY walikuwa wakitambulisha albam yao ya "HABARI NDIO HIYO" wasaNii kibao wa Bongo flava waliperfom siku hiyo.
Yote hii ilikuwa ni kazi ya STRE8 MUSIC pamoja na CLOUDS FM

FAT JOE ON DA STAGE




Mtu mzima FAT JOE akiwa kwenye kazi jijini Dar es salaam. Siku hiyo pia mwanadada EVE naye alikamua vya kutosha, siku hizi bongo kama NEW YORK

Monday, December 8, 2008

MUZIKIMNENE.BLOGSPOT.COM

TUNAPENDA KUWASHUKURU WADAI WOTE AMBAO MMEKUWA MKINITUMIA MAONI YENU, KAMA NDIO KWANZA UNAJIUNGA NASI KWENYE PAGE YETU HII NI MAAALUM KWAAJILI YAKO WEWE MSOMAJI TUTUMIE PICHA NA MAONI KUPITIA haramba29@yahoo.co.uk

PATA MANEWS YA KIJANJA BILA KUSAHAU PICHA ZA BONGO NA ZA MBELE MUZIKIMNENE NI KWAAJILI YA WABONGO WOTEE..

Friday, December 5, 2008

JOE AKICHONGA NA WABONGO




Joe Thomas akichonga na waandishi wa habari @ Kempiski siku moja kabla ya show yake na Tento Mentro na Devonte @ Leaders Club.

JOE THOMAS AKIINGIA KEMPISKI




JOE THOMAS AKIINGIA KWENYE UKUMBI KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KWENYENUKUMBI WA HOTEL YA KEMPISKI, DA ES SALAAM

Monday, December 1, 2008

JAMAICA MPAKA BONGO



Mmoja kati ya wasanii aliyepiga show ya nguvu @ Leaders Club akijulikana kwa jina la TENTO MENTRO alipokuwa akilonga na waandishi wa news wa kibongo ndani ya Kempiski in Dar.

JK FACE 2 FACE NA BAN KI MOON



JK wakibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki moon na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Augustine Mahiga huko jijini Doha.

BOYS 2 MEN WAOMBA MSAMAHA




Kundi la BOYS 2 MEN walishindwa kutokea kwenye show ya LIKIZO TYME baada ya mmoja waokuugua ghafla,,memba wa kundihilo WANYA alituma video akiomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana nakutokufika kwao kwenye show hiyo, huku akisisitiza kuwa tatizo sio promota bali ni matatizo ya kawaida ya kibinaadamu. Lkini licha ya kutokuwepo kwao JOE THOMAS pamoja na artises wengine kutoka Jamaica waliweza kuwakirisha vyema.

Wednesday, November 26, 2008

HELLO MUZIKIMNENE!!!!!




The gal anajulikana kwa jina la DYNA ni msanii wa kuimba akiwa anatokea pande za Dodoma, hapa alikuwa katika pose, kwa sasa anatamba na ngoma yake aliyompa shavu Marlaw. Kaa tayari kujua mengi kuhusu mrembo huyu kupitia hapahapa muzikimnene.blogspo.com

Tuesday, November 25, 2008

DR LOVE WA MAGIC FM & TIRA WA TRIPPLE A FM


Niky Ngonyani wa Magic FM akiwa anabadilishana mawazo na Tira Philip aka TIFEE pandee flani za Arusha siku ya uzinduzi wa Magic FM (98.6 FM)tarehe 15 November 2008 maeneo ya Masai Camp.

Monday, November 24, 2008

MACHINGA MPAKA KWENYE MAGODORO!!!




Vijana wa kitanzania wakiwa katika purukushani za kawaida za kimaisha, hapa wanaonekana vijana wawili waliokutwa na John wa muzikimnene wakiwa wanatembeza biashara ya magodoro maeneo ya Kipawa relini.

Friday, November 21, 2008

REVIEW YA OPRAH



OPRAH

WaigizajiI: Irene Uwoya 'Oprah',Ray ,Kanumba,Aunt
Mtunzi:Vicent Kigosi 'Ray'

Ray na Kanumba waliwahi soma wote shule ila walipotezana kwa muda mrefu hadi walipokutana tena Kijijini Ray akiwa mambo safi huko Kanumba akiwa choka mbaya,Ray akaamua kumsaidia Kanumba kwa kumchukua na kwenda ishi nae kwake ambako aliahidi mtibia kwania alikuwa anaumwa na kumsomesha ili aweze jiendeleza.

Oprah ambaye ni mke waRay hakupenda ujio wa Kanumba nyumbani kwake na alionyesha chuki za wazi wazi hadi siku yake ya kuzaliwa mabpo Kanumba alimzawadia zawadi ya ua na kuonyesha anamjali kuliko hata mumewe ndipo roho yake ilipomdondokea na kuanza kumtega kimapenzi ambapo kanumba nae alinasa.

Kama ujuavyo penzi ni kikohozi kulificha huwezi mapenzi yao yalikuwa yawazi yaliyopelekea mfanyakazi wa ndani kuyastukia na hadi Oprah kujua wameshajulikana na kuanza mfanyia visa ili aondoke ndani ya ile nyumba

Japo Ray alikuwa anapinga kuondoka kwake ila mwisho wasiku visa vilizidi kwani Opra alimuondosha kwa nguvu kwa kumchukua na kumsafirisha bila lumhirikisha Ray

Nae House Girl hakutaka ondoka hivi hivi alimpigia Ray siku na kumwekeza kuwa kuna barua amemuachia nyuma ya fremu ya picha ambayo ndo ina kisa cha yeye kuondolewa nadani yanyumba ile na mkewe Oprah

Ray alienda ifuata ile barua na alipofika ofisini aliifunga nakusoma ndo alipokuna barua ikieleza kigana ubaga mapenzi ya Oprah na Kanumba na kumuamuru mkewe asitoke nyumbani amsuri anarudi

STARS FANYENI MAMBO BWANA



Stars inabidi mwendeleze kukaza jabo hata tupate droo kwenye game linalokuja la marudiano ili tuwape watanzania raha, wajamani kwani sisi tunanini mpaka tuwe tunakosa kila siku utadhani tuna lala na bundi.
STAR TIMU KANDAMIZA SUDANI 4-0 TU ZINATOSHA WAENDE KWAO WAKAENDELEZE ,,hivi Sudani ni maarufu kwanini vile?????

NYOMI LA MAGIC FM






Nyomi la R-Chuga (Arusha) siku ya uzinduzi wa MAGIC FM huko kwenye mji wa baridi ambao zamani tulizoea kuuita half London.