Hivi unamkubuka huyu jamaa??? kama utakuwa ni mfuatiliaji kiasi wa muziki wa BONGO FLAVA utakuwa unamkumbuka, Jamaa anaitwa SAADAT aliwahi kutamba sana kupitia wimbo wake wa "Haiwezekani" aliokuwa kamshirikisha Mr BLU, wimbo ambao ulitengenezwa kwenye studio ya G Records.
Hivi sasa anasema anatarajia kurejea na ujio mpya kwenye game lakini this time anakuja sio msanii wa kurap pekee bali pia atakuwa anaimba kama unavyomchek akiwa kakamatilia gitaa akimwonyesha JOHN wa muzikimnene jinsi alivyofit kwenye gitaa.
Haya bwana sisi tunangojea ageuke,,aahh ahh No tunangoja ujio wako mpya kaka.
No comments:
Post a Comment