Monday, December 15, 2008

OYE OYE TAIFA STARS




Baada ya miaka 28 Taifa Stars imefanikiwa kuwakilisha tena kwa kufanikiwa kuidunga Sudan jumla ya magoli 5-2 nakufanikiwa kutita kwenda kucheza kwenye mashindano ya Afrika yanayohusisha wachezaji wa ligi za ndani za Afrika pekee zitakazofanyika mwezi wa saba mwakani huko Ivory Coast.
Mara ya mwisho kwa timu ya taifa ya Tanzania kucheza mizhuano ya Afrika ilikuwa mwaka 1980 huko Lagos, Nigeria (Du hii ni kali hata mimi John nilikuwa sijazaliwa).
Katika mechi ya kwanza Stars ilishinda 3-1 na mechi ya marudianao iliyofanyika Sudani Stars imeshinda 2-1. Kwa niaba ya washkaji zangu wanaonisababisha mimi nikaweza kuwaletea haya maujanja ya MUZIKIMENENE ,,naipongeza Taifa Stars na wote waliosababisha ushindi huo

No comments: