Monday, October 27, 2008

MTOTO WA MADONNA KURUDI AFRIKA?



David Banda mtoto aliyeasiliwa na mwanamuziki mahiri na mkongwe Lady Madonna nchini Malawi yawezekana akarudi kwa wazazi wake baada ya baba yake mzazi aliye nchini Malawi kueleza kuwa na fikra hizo baada ya kubaini kuwa ndoa ya ngwiji huyo wa miondoko ya POP imevunjika. Baba mzazi huyo anayejulikana kwa jina la Yohane Banda amekaririwa akisema kuwa amekuwa akimwona mtoto wake kwenye vyombo vya habari akizunguka huku na kule kitu ambacho kinampa wasiwasi.
Madona na mumewe Guy Ritchie waliofunga ndoa mwaka 2000 walitangaza kutalikiana hivi karibuni.
“Madona aliniahidi kuwa atamtunza mwanzangu vizuri na na katika mazingira ya kama mtoto wake wa kumzaa alikini kwa hali iliyo hivi sasa naanza kupata wasiwasi

No comments: