Monday, October 27, 2008

MISTARI BADO NIPO NIPO


Artise: Mwana FA
Song: Bado niponipo

chorus

MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana) * 2

MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?



Verse 1

Japo natokea Tanga mapenzi yalipozaliwa

Sijivishi ufundi nikajifanya nayajua

Mi nna akili timamu naona tu mnavyoyarukia

Ukiniona na demu mzuri haimaanishi ndio ntamuoa
Napata wakati mgumu washkaji wanapolia kwa uchungu

Kwani na mi nna maumivu yangu nasema tu na moyo wangu
Watu wanalalamika wanavyoumizwa na ndoa zao
Wengine wanaficha wanakufa na maumivu yao
Sioi leo,sioi kesho-kutwa wala mtondogoo

Sioi mchana,sioi jioni,usiku wala majogoo

Morale nliyonayo sasa siwezi kubali kuibiwa

Ngoja nizeekezeeke kwanza pengine ntakuja elewa

Eti nizibe maskio
Wengine nifumbe macho

Nisione wakati naibiwa?

Hamuwezi kuwa hamjalewa

Mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi

So miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini



Chorus…



Verse 2

Hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani?

Watu wana watu wao wengine toka zamani
Ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako

Wadogo usoni wanahifadhi wazee wako

Sijui ni dhiki au tamaa tu??

Watoto wanaanika njaa tu

Hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu

Msinipe headache/staki kufuata Mkumbo

Nyi anzeni mi niacheni,staki
kufanya gamble
Marafiki wanauzana/ndio zao vicheche

Na daima wanateteana/usiwaamini usiniangushe

Anataka kuolewa na anamegwa kama kawa

Demu wako akiuza wenzake,zinduka nae analiwa/yes’

Staki kuoa sababu staki kulia
Najipanga nisiharibu staki mje kunihurumia

Nafahamu nna Bahati mbaya kama nalala na bundi

Ndio maana sijipi moyo wala sijitii maufundi

Alilala na bibi arusi/siku moja kabla ya arusi

Na wala sio bwana arusi/bado mnanishauri arusi?

Eti nizibe maskio
Wengine nifumbe macho
Nisione wakati naibiwa??

Hamuwezi kuwa hamjalewa



Chorus….



Verse 3

Usiseme unaamini mwanamke hata kama unamtania

Watu na akili zao washajichuuza na wakalia

Sikatazi watu kuoa

Na hata nikiwakataza neno langu sio sheria

Sipendi wanawake napenda wanawake wazuri

Wanaojitunza wanajiheshimu sio wa simu na gari

Inahitaji muda kuwapata hakuna anaewajua vizuri

Ndio maana mi nipo nipo sitaki kuvamia shari

Wanatoroka na wazungu/wanamegwa na vibabu

Wanaiba waume za wenzao uso mkavu hawana aibu

Ukitaka wako peke yako labda umuumbe mwenyewe

Au kata mgonjwa uufiche mtaani usishindaniwe

Wakikumegea demu wako nawe tafuta mnyonge ummegee

Haipunguzi maumivu inarudisha hadhi ya kiume

Kumegewa ni jambo moja kukimbiwa ushafkiria??

Sio kila demu umuonae unaweza muoa

Eti nizibe maskio
Wengine nifumbe macho

Nisione wakati naibiwa??

Hamuwezi kuwa hamjalewa

Mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi

So miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini


Chorus…

Outro..

Yes yes…it’s yo boy FA
Na Hermy B..ni kazi chafu but lazima mtu aifanye

Sipendi wanawake napenda wanawake wazuri

Wanaojitunza wanajiheshimu sio wa mkwanja na gari

Yeeeeah,love is love my people 
Ladies,behave basi/…au sio??

No comments: