Sanaa ya ubunifu inazidi kukua ndani ya Bongo, tukiwa tumezoea kusikia majina ya wabunifu kama Masoud Kipanya, Mustapha Has anal na wengineo wengi sasa kizazi kipya kinakuja kwenye game. Giovanni Di Piazza mbunifu chipukizi aliyeanza kuonyesha makali yake kwa kubuni T-Shirts zenye chata ya mgombea uraisi wa USA 2008 kupitia chama cha Democrat Barrack Obama.
Designer huyu mwenye asili ya kiitaliano (upande wa baba) na kitanzania (kwa mama) amesema baada ya kuona mafaniki kutoka kwa kazi yake ya kwanza hiyo aliyoifanya anatarajia kuingia deep zaidi kwenye fani hiyo kwa kuanza kubuni nguo zitakazo kuwa na logo yake ya Di Pizza.
Kwa sasa nguo zake zenye chata ya Obama zinapatikana Mlimani Classic wear, Zizou shops na pia yeye mwenyewe anazitembeza mkononi.
No comments:
Post a Comment