Wednesday, October 22, 2008

CHAMPION OF CHAMPIONS




Japhet Kaseba yupoJapani kwenye competition ya kickboxing, japo alichelewa kufika huko kwaajili ya matangazo lakini alifika kabla ya competition kuanza rasmi. Pambano lake la kwanza aliumia goti na kusababisha akae nje ya ulingo kwa muda akisubiri kupona, God kampa nguvu kapona na amerudi tena mchezoni

Akiongea na muzikimnene, Kaseba amesema “Nimefanikiwa kuongea na Promoter Mkuu wa K 1 kwa ajili ya kuja kuanzisha K 1 AFRICA kama ilivyoanzishwa K 1 ASIA, K 1 EUROPE na K 1 AMERICA na amekubaliana na mimi kuja kunisaport na hivyo nategemea kuleta fighters wa K 1 kuja kupigana na Kick Boxers wa East Africa mipango imeshaanza kupangwa”

“Natarajia itakuwa December 2008 nategemea kurudi mwezi wa 11 kuja kuweka mambo sawa ya mechi baada ya mechi nategemea kurudi tena Japan kuendelea na Mashindano ya K 1”- Kaseba.

No comments: