Wednesday, October 22, 2008

CHEKA KIMTINDO!!

UNATAKA KUJINYONGA???
Kuna msela alikuwa ghetto amechill full stressed, kafikiria akaona kama vipi isiwe inshu ngoja ajimuvuzishe kwa sir God, lakini kabla hajafanya hivyo akakumbuka kuna mshkaji wake kipenzi ambaye amekuwa akimpa ma-advice pindi apatapo mitihani kama hiyo.

Akamcall “Oyo mwana mimi nataka kujinyonga maana naona maisha yamezidi kuwa magumu kilasiku naona isiwe tabu, sasa kabla sijafanikisha malengo yangu naomba ushauri wako”

Rafiki yake akamjibu hivi “Haina noma mwana wewe jinyonge tu maana maana matatizo yamekuzidi ila kabla unafanya hivyo naomba unikabidhi ATM Card yako, Laptop yako, vyeti vyako, salio la hela yako yote uliyonayo na zile nguo ulizotumiwa kutoka Marekani baada ya hapo endeleaaa!!!”

No comments: