Friday, October 31, 2008

NIAJE!!!!1



I go by the name J.J. HARAMBA....HEKO KWA muzikimnene

HAPO VIPI?


MB Dog alishaimba haya mapenzi ni kitu gani......Cheki ni na hii mwana kisha niambie hapo vipi

THE MAN HIM SELF FROM TIME FM



Jacob Mhina aka DJ KOBO koja kati ya DJ mwenye skillz za kutosha kutoka TIMES FM akiwa kwenye pose maeneo ya kwao pande flani za Ukonga.. Kobo anasema DJz wengi wa kibongo hawaumizi vichwa kujifua kwa mazoezi na ndio maana wanakosa skills za ukweli.
"Mimi nafanya mixing za ukweli muziki wa aina zote sichagui na hakuna siri zaidi ya mazoezi kwa sana, utundu huu niliuanza zamani tangu nikiwa home natumia mashine za mshua" alisema Kobo aka Baba Martha

Wednesday, October 29, 2008

T.I STILL ANATESA



T.I. still anashikilia chat za media tofauti tofauti kwa takribani wiki ya saba sasa huku akiwa anapata challange ya kugombania nafasi hzi na wanadada Beyonce na Rihanna. Single ya “Whatever You Like” pia single ya “Live Your Life” aliyompa shavu Rihanna bado zinatesa si kitoto huku Beyonce akitamba na single yake ya “If I Were A Boy.”.

AFANDE NDANI YA ULAYA



Baada ya msoto wa muda mrefu akikomaaa na muziki wa Bongo hatimaye matunda ya makamuzi yake yamezidi kuonekana mtu mzima Afande Sele amepata shavu la ukweli baada ya kupata chance ya kwenda kukamua wanakotoka kina Zizou, Henry, Viera n.k
Hiyo ni ndanio ya Ufaransa , katika tour hiyo Afande ataperform kwenye miji kumi tofauti tofauti chini ya mwaliko wa promota maarafu nchin humo anayejulika kwa jina la Michelle. Pia aka Simba Dume ataambatana na washkaji ambao ni Balleti, Juma Mjivi na Eric pamoja na DJ wake K.O.
Hii ni kwamujibu wa meneja wa K.O ambaye ni DJ wa Afande Sele

Monday, October 27, 2008

BABY & WIZZY NDANI YA MUVI




Maswali yaliyopo ni kuwa Je muzi hii itauza kweli au ndio..Cash Money Record’s CEO Bryan Williams aka Baby aka Birdman ametangaza kuwa hivi sasa yupo kwenye mipango ya kushot filam ambayo wahuzika wakuu yaani ma-staring watakuwa ni yeye na Lil Wayne na itajulikan kwa jina la “Like Father, Baby ameseama muzi hiyo wanatarajia kuwa itaingia sokoni mwezi June mwakani ambapo itaambatana na albam yao ya pamoja.

NAKAAYA & BOYFRIEND



Nakaaya akiwa na her boyfriend the man from Jamaica...Si unajua tena utandawazi wabongo tumepata shemeji Mjamaica,,, how do u see that?

WABONGO CLAN FROM TABATA


The gal known as Anna akiwa amechill kwaajili ya snap na The hater of politician Nakaaya Sumari kwenye party ya BASH COLLAGE iliyofanyika juzi side za Leaders Club

BONGO.HOME

WIZZY APATA BABYBOY


Kwa mujibu wa watu wa karibu na Lil Wayne inasemekana kuwa aka Mr make rain amepata baby boy,,,Wizzy alikaririwa wiki iliyopita akisema kuwa anatarajia kupata mtoto hivi karibuni.

NAKO 2 NAKO KAMA P-SQUARE




Baada ya P-Square kufanya kweli kupitia wimbo wa “Do Me” wana hip hop kutoka pande za A-City aka Arusha wanatarajia kuachia dude lao jipya linalojulikana kwa jina la “Do It”

Akiongea na muzikimnene moja kati ya memba wa kundi hilo Ibra Da Hustle anasema kuwa mkono huo umefanyika ndani ya Kama Kawa Records ya Dar pia mpaka sasa wameshakamilisha albam yao mpya ambayo yote imerekodiwa ndani ya wiki mbili ndani ya Bongo Records.

TOP 10 HIT



Chek chat ya pini zinazotamba kwa sasa kwenye game ya Bongo kwa sasa, kama una comments yoyote juu ya chat hii chek nasi watu wa muzikimnene kupitia haramba29@yahoo.co.uk



1. Bado NipoNipo –Mwana FA
2. Usiende Mbali - Juliana & Bushoke
3. Tutaonana Wabaya - Q-Chilla
4. Sirimba – Ngoni & Lady JD
5. My SweetLove - Wahuu
6. Nipe Dili - Ngwear
7. Salary - Nameless
8. Kidato Kimoja - JI
9. Usiniache - Spark
10. Hao – Mwasiti

MTOTO WA MADONNA KURUDI AFRIKA?



David Banda mtoto aliyeasiliwa na mwanamuziki mahiri na mkongwe Lady Madonna nchini Malawi yawezekana akarudi kwa wazazi wake baada ya baba yake mzazi aliye nchini Malawi kueleza kuwa na fikra hizo baada ya kubaini kuwa ndoa ya ngwiji huyo wa miondoko ya POP imevunjika. Baba mzazi huyo anayejulikana kwa jina la Yohane Banda amekaririwa akisema kuwa amekuwa akimwona mtoto wake kwenye vyombo vya habari akizunguka huku na kule kitu ambacho kinampa wasiwasi.
Madona na mumewe Guy Ritchie waliofunga ndoa mwaka 2000 walitangaza kutalikiana hivi karibuni.
“Madona aliniahidi kuwa atamtunza mwanzangu vizuri na na katika mazingira ya kama mtoto wake wa kumzaa alikini kwa hali iliyo hivi sasa naanza kupata wasiwasi

MISTARI BADO NIPO NIPO


Artise: Mwana FA
Song: Bado niponipo

chorus

MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana) * 2

MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?



Verse 1

Japo natokea Tanga mapenzi yalipozaliwa

Sijivishi ufundi nikajifanya nayajua

Mi nna akili timamu naona tu mnavyoyarukia

Ukiniona na demu mzuri haimaanishi ndio ntamuoa
Napata wakati mgumu washkaji wanapolia kwa uchungu

Kwani na mi nna maumivu yangu nasema tu na moyo wangu
Watu wanalalamika wanavyoumizwa na ndoa zao
Wengine wanaficha wanakufa na maumivu yao
Sioi leo,sioi kesho-kutwa wala mtondogoo

Sioi mchana,sioi jioni,usiku wala majogoo

Morale nliyonayo sasa siwezi kubali kuibiwa

Ngoja nizeekezeeke kwanza pengine ntakuja elewa

Eti nizibe maskio
Wengine nifumbe macho

Nisione wakati naibiwa?

Hamuwezi kuwa hamjalewa

Mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi

So miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini



Chorus…



Verse 2

Hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani?

Watu wana watu wao wengine toka zamani
Ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako

Wadogo usoni wanahifadhi wazee wako

Sijui ni dhiki au tamaa tu??

Watoto wanaanika njaa tu

Hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu

Msinipe headache/staki kufuata Mkumbo

Nyi anzeni mi niacheni,staki
kufanya gamble
Marafiki wanauzana/ndio zao vicheche

Na daima wanateteana/usiwaamini usiniangushe

Anataka kuolewa na anamegwa kama kawa

Demu wako akiuza wenzake,zinduka nae analiwa/yes’

Staki kuoa sababu staki kulia
Najipanga nisiharibu staki mje kunihurumia

Nafahamu nna Bahati mbaya kama nalala na bundi

Ndio maana sijipi moyo wala sijitii maufundi

Alilala na bibi arusi/siku moja kabla ya arusi

Na wala sio bwana arusi/bado mnanishauri arusi?

Eti nizibe maskio
Wengine nifumbe macho
Nisione wakati naibiwa??

Hamuwezi kuwa hamjalewa



Chorus….



Verse 3

Usiseme unaamini mwanamke hata kama unamtania

Watu na akili zao washajichuuza na wakalia

Sikatazi watu kuoa

Na hata nikiwakataza neno langu sio sheria

Sipendi wanawake napenda wanawake wazuri

Wanaojitunza wanajiheshimu sio wa simu na gari

Inahitaji muda kuwapata hakuna anaewajua vizuri

Ndio maana mi nipo nipo sitaki kuvamia shari

Wanatoroka na wazungu/wanamegwa na vibabu

Wanaiba waume za wenzao uso mkavu hawana aibu

Ukitaka wako peke yako labda umuumbe mwenyewe

Au kata mgonjwa uufiche mtaani usishindaniwe

Wakikumegea demu wako nawe tafuta mnyonge ummegee

Haipunguzi maumivu inarudisha hadhi ya kiume

Kumegewa ni jambo moja kukimbiwa ushafkiria??

Sio kila demu umuonae unaweza muoa

Eti nizibe maskio
Wengine nifumbe macho

Nisione wakati naibiwa??

Hamuwezi kuwa hamjalewa

Mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi

So miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini


Chorus…

Outro..

Yes yes…it’s yo boy FA
Na Hermy B..ni kazi chafu but lazima mtu aifanye

Sipendi wanawake napenda wanawake wazuri

Wanaojitunza wanajiheshimu sio wa mkwanja na gari

Yeeeeah,love is love my people 
Ladies,behave basi/…au sio??

Sunday, October 26, 2008

HII SI HATARI JAMANI!!!



Hii ni sehemu moja wapo ya kituo cha daladala maeneo ya Manzese kikiwa katika hali mbaya kwa kuonyesha dalili za kuanguka, hali inayotishia amani ya watumiaji wa kituo hicho.

Saturday, October 25, 2008

Thursday, October 23, 2008

JAMANI ZUMA ANA MKOSI GANI TENAA

Hakimu mmoja wa Afrika Kusini amewapa ruhusa waendesha mashitaka kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyomfutia kiongozi wa chama tawala wa nchi hiyo Jacob Zuma madai ya kuhusika na ufisadi.
Mwezi uliopita, hakimu Chris Nicolson alifuta mashitaka yaliyokuwa yakimkabili Bw Zuma.
Hakimu huyo alipendekeza kwamba mpinzani wake aliyekuwa rais wa nchi hiyo Thabo Mbeki aliingilia kesi hiyo.
Hukumu hiyo ilitoa fursa kwa chama tawala cha African National Congress, ANC kumwondosha Bw Mbeki madarakani.

UCHAGUZI WA USA


Mahasimu katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais nchini Marekani wamezidi kukosoana kuhusu mipango yao ya kufufua uchumi endapo watachaguliwa kuingia madarakani.
Wanasiasa hao wameelekeza nguvu zao kwenye majimbo muhimu ambayo kura za wajumbe wa kumchagua rais mara nyingi huamua mshindi.

JUA KALIIIII


Wakazi wa Kipawa wakila msoto kwenye jua kituoni baada ya sehemu ya kupumzikia kubomoka na kisha wajanja wa mjini wakasepa na mabati na nila kitu hali inayofanya wakazi hao kukosa sehemu ya kupumzika wakati wakisubiri daladala.

THE DAN DADA aka BLACK RHINO

Black Rhino akiwa kwenye pose alipokuwa akichonga na muzikimnene

Wednesday, October 22, 2008

BONGO MNA FEEL AJE



Una

mkumbuka jamaa aliye shine na noma ya Unafee aje,, sasa yeye akiwa pamoko na artistes wengine wa hip hop kutoka pande za Kenya wamefanya bonge moja la kolabo pia umo ndani kuna BLACK RHINO amekamua kisawasawa...tega sikio...

BLACK CHATA NJIANI MTV & CHANNEL O





Young bro wa Prof Jay Black Rhino amewaomba fans wake wampe sapoti kwa kununua albam yake ya kwanza iliyo sokoni go by ze name “USIPIME” yenye ngoma 10. Akiongea na muzikimnene Black ambaye kwa sasa yupo juu kupitia pini lake la “BLACK CHATA” amelonga kuwa hatarajii kuacha kufanya HIP HOP katika life yake yote ya kimuziki.
Mwanazuoni huyu wa MZUMBE UNIVERSITY yupo kwenye harakati za kushot video za ngoma zake nyingine zilizo ndani ya albam hiyo ikiwemo "Najuua Nimekosa" ft Enika.
“Pia nipo kwenye process za kupeleka video ya “BLACK CHATA” kwenye vituo cha Channel O na MTV baada ya hapo nitaanza kudili na my next project”alisema Rhino

YANGA VS SIMBA


MWANAWANE JE MNYAMA ATAANGUKA AU ATAENDELEZA UBABE,,,NIPE MTAZAMO WAKO...

CHAMPION OF CHAMPIONS




Japhet Kaseba yupoJapani kwenye competition ya kickboxing, japo alichelewa kufika huko kwaajili ya matangazo lakini alifika kabla ya competition kuanza rasmi. Pambano lake la kwanza aliumia goti na kusababisha akae nje ya ulingo kwa muda akisubiri kupona, God kampa nguvu kapona na amerudi tena mchezoni

Akiongea na muzikimnene, Kaseba amesema “Nimefanikiwa kuongea na Promoter Mkuu wa K 1 kwa ajili ya kuja kuanzisha K 1 AFRICA kama ilivyoanzishwa K 1 ASIA, K 1 EUROPE na K 1 AMERICA na amekubaliana na mimi kuja kunisaport na hivyo nategemea kuleta fighters wa K 1 kuja kupigana na Kick Boxers wa East Africa mipango imeshaanza kupangwa”

“Natarajia itakuwa December 2008 nategemea kurudi mwezi wa 11 kuja kuweka mambo sawa ya mechi baada ya mechi nategemea kurudi tena Japan kuendelea na Mashindano ya K 1”- Kaseba.

LOVE IS.......


Unakumbuka makamuzi ya wadada hawa,,,hivi wabongo nasisi hatuwezi kufikia levo hizi? hakika tunaweza bwana kazeni buti

JOSE NA BOBBY


Baada ya kupata ajali ya kuanguka kutoka kwenye flat huko Arusha alipokuwa kwenye harakati za kufanya show maalum kwaajili ya Fiesta na kupelekea kuvunjika miguu yake.
Hivi sasa Jose Chameleon anaendelea vizuri kiasi na katika hali ya kushangaza wengi ,,last week hasimu wake mkubwa kwenye muziki nchini Uganda Bobby Wine aliweka chuki ya muziki pembeni na kwenda kumtembelea hospitalini,,Josee alifurahi sana na wameongea mengi baada ya kitambo kirefu.

CHEKA KIMTINDO!!

UNATAKA KUJINYONGA???
Kuna msela alikuwa ghetto amechill full stressed, kafikiria akaona kama vipi isiwe inshu ngoja ajimuvuzishe kwa sir God, lakini kabla hajafanya hivyo akakumbuka kuna mshkaji wake kipenzi ambaye amekuwa akimpa ma-advice pindi apatapo mitihani kama hiyo.

Akamcall “Oyo mwana mimi nataka kujinyonga maana naona maisha yamezidi kuwa magumu kilasiku naona isiwe tabu, sasa kabla sijafanikisha malengo yangu naomba ushauri wako”

Rafiki yake akamjibu hivi “Haina noma mwana wewe jinyonge tu maana maana matatizo yamekuzidi ila kabla unafanya hivyo naomba unikabidhi ATM Card yako, Laptop yako, vyeti vyako, salio la hela yako yote uliyonayo na zile nguo ulizotumiwa kutoka Marekani baada ya hapo endeleaaa!!!”

Monday, October 20, 2008

MAMABO YA USA HAYA


Basi la uchaguzi la BBC likikata mitaa katika jiji la New York baada ya kuwasili likitokea jimbo la Pennsylvania kupitia New Jersey kukamilisha safari yake ya kilometa zaidi ya 11,000.

SISTA DO AKITAFAKARI USAFIRI POSTA!!


CARTER 4 ?????


Kwa mujibu wa MTV News, inasemekana kuwa mtu mzima Lil Wayne yupo studio akirekodi tracks za albam yake ijayo. Ilidaiwa kuwa mara baada ya kurelease albam zake zilizopita kwa jina la THE CARTER 1,2 & 3 Wayne alisema kuwa huo ndio mwisho wa albam zake kujulikana kwa jina la Carter alkini inadaiwa kuwa mzigo huo unaotarajiwa kuachiwa mwakani pia unaweza kujulikana kwa jina la THE ARTER 4….KAMA VIPI TUSUBIRI TUONEEE

MUVI YA LUDA YASHIKA NAMBA MOJA


Muvi inayojulikana kwa jina la Max Payne ambayo rapa wa michano ya hip hop Christopher Bridges aka. Ludacris ni kati ya wahusika wakuu imefanya vizuri katika chat za Weekend’s box office kwa kushika namba moja. Muvi hiyo iliyokuwa imetengewa bajeti ya dola millioni 35 za kimarekani pia imewahusisha Mila Kunis, Chris O’Donnell, na Beau Bridges kama wahusika wakuu.

CHEKA NA MUZIKIMNENE

MOSHI WA A-TOWN NOMA

Kuna washkaji watatu walikuwa wamechill kwenye chumba flani hivi wanapuliza kitu cha A-City aka Majani, basi bwana mjani ukiwa umekolea kibiriti walichokuwa wakikitumia kikawa kimeisha na still walikuwa wanakihitaji kukitumia ikabidi wamtume mwenzao mmoja kwenda kutafuta kibiriti, mchizi hakupinga ikabidi atoke nje kwenda kuatafuta kibiriti.
Mchizi alipofika nje akazunguka nje ya nyumba hilehile waliyokuwemo kisha akarudi kwa wale wale wana wake alipowakuta akaanza kusemesha huku akiwa anayumba yumba “Oya eehe machizi naombeni kiberiti kama kuna mtu anacho kati yenu?”Wale wawili waliokuwa wamekaa wakamjibu “Kuna mwenetu mmoja ameenda kuazima hapo jirani kama vipi njoo tumsubiri atarudi muda sio mrefu”.

VIONGOZI WA JIJI MPO!!!


Watu kama hawa wanatakiwa kuwa na vifaa maalum kwaajili ya kufanikisha kazi zao lakini chek mama huyu, alikutwa na muzikimnene maeneo ya Moroko kituoni akisafisha barabara bila kuwa na vifaa byoyote vya kumkinga na vumbi nk.

Saturday, October 18, 2008

MUZIKI MNENE

Inakuwaje wana karibu katika blog yetu wakubwa kwa wadogo, wazee kwa vijana, wake kwa waume, hapo nadhani nimemaliza au kuna levo nilizozivuka?? I hope hakuna!! Kama blog yenyewe inavyojieleza muziki mnene ni kweli muziki ni mnene usiupimie!!
Chaguo ni lako tu, mazaga ni mengi yaliyosheheni full maujanja kutoka kona zote za dunia kwenye Entertainment, siasa, jamii na mengine mengi ikiwemo kuchat, news, matukio, vichekesho n.k
Pia unaweza kutumuvuzishia pichazz, comments zako, opinions & anything u want 2 share wit us ila mwanawane matusi na picha zisizofaha hazina chance kabisa katika blog hii. KARIBUNI WOTE & ENJOY

TWANGA KAMA KAWA



Moja kati ya bendi za kitambo kwenye game ya muziki wa BongoTwanga Pepeta wamesema hawatarajii kuachia wimbo mwingine kwenye media isipokuwa tu watakapokuwa tayari kuuza albam hiyo.

Akilonga na muzikumnene Mkurugenzi wa bendi hiyo mama Komando aka Asha Baraka amesema wataendelea kuzitumia nyimbo zao mpya kwenye show pekee na si vinginevyo.

MZIGO MKUBWA NDANI YA BONGO




Jamani eehh hivi si tuliamabiwa kuwa magari makubwa yanakuja halafu vipanya viondoke katikati ya jiji sasa mbona ndinga zenyewe zinaonekana kimachale ?

Hii ilikutwa na muzikimnene ikisanya routs ya Kariakoo to Mbagala

HIINDIO BONGO!!




Hii kwetu Bobgo ni kawaida kwa sana,,,si unamcheki msela katikati ya jiji akiyasongesha maisha na yeye mwenyewe akisema hapo life bora kama yalivyo kwa wa Tz wengine.

THE GAME KUTOA DVD YA MAISHA YAKE



Imezoeleka kwa fans kibao kutaka kujua life style ya ma-celeb wao iwe ni kwa bongo au mbelembele.. sasa ikiwa unataka kujua personal life ya mtu mzima THE GAME (former memba wa G-Unit) anatarajia kurelease DVD ambayo itakuwa ikielezea maisha yake tangu alioanza kupata umaarufu mpaka levo alizopo kwa sasa..Umo ndani kuna mastaa wengine kibao baadhi yao ni Snoop Dogg, Kanye West, Katt Williams, Dr. Dre na 50 Cent.
Black Wall Street ndio waliohusika kwenye suala zima la production. Kama vipi unamfeel mchizi ikitoka tu we ruka nayo au vipi mwanaaa!!

BONGO FLAVA NDANI YA PAM AWARDS




Ikiwa ni mfuatiliaji wa muziki huu kitu hiki sio mara ya kwanza kussikika masikioni mwako, wasanii wa bongo flava wapo kwenye nomination ya tuzo za UG. I hope na wengi wanu mtakuwa mmenisoma ikiwa hunihelewe habati ni hivi. Wasanii Professa Jay, AY, Bushoke na Mr Nice wamo kwenye nomination ya tuzo za PAM kwenye kategori ya Msanii Bora Wa Kiume kutoka Tanzania
Muzikimnene ilipoongea na Ambwene Yessayah aka AY amesema ili kumpigia kura unachotakiwa kufanya ni kuandika sms yenye neno “32 AY” kisha unatuma kwenda namba +255 782 601 481.
AY amesisitiza kuwa anawaomba sana waTZ wampe sapoti kama ambavyo wamekuwa wakimpa.

ETI RICHARD HAKUWAHI KUUANGALIA BBA!!



Yawezekana usiamini habari hii lakini ukweli ndio huu, hivi ni nani Bongo hii asiyeujua mchezo wa BIG BROTHER AFRICA unaofanyika kila mwaka mara moja huko SAUTH AFRICA wengi wetu tunafahamu kuwa wabongo wenzetu Mwisho alikamua vyema na kushika namba mbili pia Richard mwaka jana ndiye aliye ibuka baba lao akiwa ndiye top kabla ya mwaka huu dada (Latoya) yetu alipo bolonga , lakini hiyo siyo story.
Story ni kuwa bingwa huyo wa mwaka jana anadai kuwa kabla ya kujiunga kwenye mchezo huo kumbe hakuwahi kuangalia BIG BROTHER ya mara ya kwanza hata siku moja “Unadhani mshkaji wangu mimi sikuwahi kuangalia mchezo wa kina Mwisho hata saiku moja ila nilivyosikia kuna chance mi nikazamia tu bila hata kujua nini kinatakiwa si unajua tena mimi ni mbishi wa maisha” alisema Richard Bezuidenhout alipokuwa alikonga na muzikimnene.
More about him chek through his web
www.richardbba2winner.com

BONGO MNAM-FEEL OBAMA!!




Sanaa ya ubunifu inazidi kukua ndani ya Bongo, tukiwa tumezoea kusikia majina ya wabunifu kama Masoud Kipanya, Mustapha Has anal na wengineo wengi sasa kizazi kipya kinakuja kwenye game. Giovanni Di Piazza mbunifu chipukizi aliyeanza kuonyesha makali yake kwa kubuni T-Shirts zenye chata ya mgombea uraisi wa USA 2008 kupitia chama cha Democrat Barrack Obama.
Designer huyu mwenye asili ya kiitaliano (upande wa baba) na kitanzania (kwa mama) amesema baada ya kuona mafaniki kutoka kwa kazi yake ya kwanza hiyo aliyoifanya anatarajia kuingia deep zaidi kwenye fani hiyo kwa kuanza kubuni nguo zitakazo kuwa na logo yake ya Di Pizza.
Kwa sasa nguo zake zenye chata ya Obama zinapatikana Mlimani Classic wear, Zizou shops na pia yeye mwenyewe anazitembeza mkononi.

BONGO TOP10

Kwa wale ambao wapo anga za mbali au hata kama upo Bongo hizi ni Top 10 Bongo Flava zinazotamba kwa sana Bongo. Zipo nyingi ambazo zipo juu lakini muzikimnene imezichagua zifuatazo:


1. Bado NipoNipo –Mwana FA

2. Usiende Mbali - Juliana & Bushoke

3. Sirimba – Ngoni & Lady JD

4. Tutaonana Wabaya - Q-Chilla

5. Ndoa Haina Doa – Inspector Haloun

6. Kidato Kimoja - JI

7. Usiniache - Spark

8. Hao – Mwasiti

9. Nipe Dili 0 Ngwear

10. Dunia Njia - Bushoke


Friday, October 10, 2008