Tuesday, December 1, 2009

NIMEHAMIA GAZETI LA CHAMPIONI KWA SASA

Mambo vipi wazeyaaaaa nipo kwenye mishe misheza kuhama so sijatulia lakini msikonde baada ya muda fulani kila kitu kitakwenda sawa...kwa sasa sipo tena TANZANIA DAIMA na SAYARI...nimehamia kwa wajanja wa town kwenye gazeti la CHAMPIONI kama vipi nitawajulisha kila kitu kuhusu job yangu mpya....
John Joseph

Saturday, November 21, 2009

RATIBA YA WIKI YA BILICANS


Bilicanas Weekly Program

Wednesdays-
• Ngoma Afrika
• Entrance-5,000 tsh.
• Entertainment- Live Band, Dance Group

Thursdays-
• Ladies Paradise
• Entrance Ladies Free and Gents 5,000 tsh. With 5,000 drink coupon.
• Entertainment- Band + other entertainment.

Fridays-
• Zain Wonders Party
• Entrance 10,000 tsh
• Entertainment-Dancers and Dance Cages, Guest Djs/Competitions- Sexy Street Fashion Show- Extreme Pleasure All Night!!

Saturdays-
• Crazy Saturday Night Live with East Africa
• Entertainment-Live Video Mix- Dance Performance (MJ)-Dance Competitions and Mc Competitions + Dancers and cages. Pure Ecstasy!
• Entrance 10,000 tsh

Sunday-
• Way Back Sundays
• Live Band and Old School Sundays
• Entrance 5,000 tsh
• Entertainment-Live Band, Dj Music.

HAINA KUSHANGAA



Huyu jamaa kwao ndiyo HANDSOME

HII NDIO BONGOOOO!!!



Haina kushangaa, gari inaenda huku mlango unabaki nyuma....

MWANAMBOKA KUWAONGOZA WENZAKE JUMAPILI HII



Na John Joseph

TAMASHA maalum la watoto linalojulikana kwa jina la Red Ribbon Children's Day linatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kesho kutwa kwa kushirikisha wanamitindo kadhaa maarufu wa hapa nchini.

Katika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House (TMH) Khadija Mwanamboka ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, alisema wabunifu hao wameamua kushiriki ili kutoa burudani kwa watoto ili kuwaonyesha jinsi wanavyowajali. Pia alisema watakuwepo wasanii wa muziki wa kiazazi kipya watakaosindikiza shughuli hiyo.

Wanamuziki hao ni Marlaw, Hemed, Profesa Jay, Mo Racka, Matonya, Chid Benz na Quick Rocka ambao watataoa burudani kwa watoto na wengineo watakaofika siku hiyo kushuhudia.

Aidha alitaja wanamitindo wengine watakaokuwepo siku hiyo na kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki ni Mustafa Hassanali, Ally Remtullah, Franko, Zamda George, Farha Sulatan na Asia Idarous atakaecheza ngoma ya kizanzibari itwayo ‘Bomu’.

Pia kutakuwa na mashindano ya kuimba na kucheza na zawadi nyingi zitatolewa kwa watoto. Sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo ni Clouds FM, Channel TEN, Entertainment Masters, Profesa Jay Foundation, Tanzania House of Talent (THT), Mokasi Medical System, Cool Blue na Shear Illusion.


MWISHO

Friday, November 20, 2009

MPOKI WA ZE KOMEDI APATA AJALI NA KUVUNJIKA MKONO



Mpoki, mwigizaji maarufu wa kundi la Ze Original Komedy (kulia) amepata ajali ya gari usiku wa kuamkia jana, na inasemekana amevunjika mkono wake wa kushoto ambapo mfupa umeachia.
Habari kutoka ndani ya kundi hilo zinasema hali yake sio mbaya sana na jana aliruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali ya Kairuki iliyoko mikocheni jijini Dar, na ataendelea na matibabu akiwa nyumbani.
Ajali hiyo ilitokea mikocheni wakati gari alilokuwa anaendesha lilipogongana uso kwa uso na Rav4 iliyokuwa inaendeshwa na mwanamama ambaye naye kalazwa hospitali ya TMJ.

Sunday, November 15, 2009

JOHN JOSEPH HARAMBA NA WADAU TUKIJIACHIA



Hapa mtu mzima nilikuwa na washkaji na wafanyakazi wenzangu tukijiachia, ilikuwa ni furaha tupu ndani ya BILICANAS

SEVEN NA SALEH ALLY



SEVEN AKIYARUDI NA SALEH ALLY KWENYE WELCOME PARTY YA ELIZABETH WA BIG BROTHER KWENYE UKUMBI WA BILICANAS

HATA MIMI NIMO !!!



Hata mimi mdau wenu JOHN JOSEPH nilikuwepo na dada Lucy Kiwere...mnamkumbuka??

ELIZA IF U DO ME I DO U



MAMBO YALIKUWA SIO MCHEZO!! HAPA ELIZABETH ALIKUWA AKICHEZA HUKU AMEZYNGUKWA NA WADAU KIBAO...

ELIZABETH WA BIG BROTHER AKIYARUDI MANGOMA



\Mwakilishi wa TANZANIA katika shindano la Big Brother, Elizabeth Gupta akiwa anayarudi mangoma katika sherehe maalum ya kumkaribisha iliyofanyika kwenye ukumbiwa BILICANAS mwishoni mwa wiki hii... mambo yalikuwa sio mchezo

NAOMI NDANI YA BONGO.



Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Marekani Naomi Campbel akiwa ndani ya Bongo hivi karibuni.

JK AKIWA NA JD NA G. HABASH



Judith Wabura aka Lady Jay Dee akiwa pamoja na Jakaya Kikwete pamoja na mumewe Gadner G. Habash wakati wa hafla ya MO Ibrahimu iliyofanyika Dar es salaam mwishoni mwa wiki huu

RAIS WA FIFA vs RAIS WA NIGERIA



Rais wa FIFA, Joseph Sepp Blatter (kushoto) akikabidhi medali ya FIFA KWA Rais wa Nigeria , Umaru Yar'Adua mnamo Novemba 15, katika mji wa Abuja.

MWENDO WA MAUZO KWA KWENDA MBELE



Mshkaji wangu anayepiga mzigo katika kituo cha MLIMANI TV, akiwa kwenye pozi na kombe la Ligi Kuu ya England.

KOMBE LA BARCLAYS LIKIWA NA WABONGO



Kombe la ligi kuu ya soka ya England lilipotua Bongo, fans kibao walijitokeza kupokea Kama wanavyoonekana baadhi ya wadau wakipozi kwaajili ya picha.

HUZUNI UJERUMANI



Wachezaji wa soka wa Ujerumani wakibeba jeneza lenye mwili wa kiwa wa nchi hiyo aliyejiua wakati wa kuuaga mwili wake.

Thursday, November 12, 2009

ELIZABETH GUPTA AKIINGIA BONGO



Elizabeth alipokuwa kiikanyaga ardhi ya Bongo mara baada ya kuwasili Jumatano ya wiki hii.

ELIZABETH AKIWASILI BONGO



Mshiriki wa Tanzania aliyekuwepo kwenye jumba la Big Brother akiwasili kutoka Afrika Kusini alipokuwa akishiriki baada ya kutolewa kwenye kinyang'anyiro hicho wiki iliyopita. Hapa likuwa amemkumbatia mtoto wa mmoja kati ya ndugu zake wealiofika kumpokea uwanja wa ndege

Sunday, November 1, 2009

MB DOG YUPO NJIA PANDA



KUMEKUWA na taarifa kuwa MB Dog aliyejitoa katika kundi la Tip Top CONNECTION yupo njia panda kuhusu kurejea kundini au la kutokana na kuyumba katika kujisimamia kazi zake. Tangu alipotoka kundini mwaka jana hajatoa albamu nyingine tangu ile ya kwanza ya ‘Ratifa’ aliyokuwa chini ya Tip Top.

UNIQ MODOZZ KUPATIKANA BONGO



MMOJA kati ya wadau wa urembo nchini Taji Liundi ambaye anamiliki mtandao wa komputa wa modotz.blogspot.com, ameandaa shindano la kuwapata wanamitindo chipukizi mchakato utakaofanyika hivi karibuni na kujulikana kwa jina la Uniq Modo.

Akielezea mchakato huo alisema hawatozingatia kimo cha washiriki tofauti na dhana iliyopo kuwa mwanamitindo lazima awe mrefu. “Hata kwa wale ambao hawatabahatika kushinda, tutahakikisha inawajali kwa kuwatafutia kazi mbalimbali za uanamitindo kwa wale watakaoonyesha kuwa na nia ya kujiendeleza kwenye fani hiyo.” alisema

Alifafanua kuwa shindano la Uniq Modo ni mwanzo wa safari ndefu ambayo itafungua njia kwa vijana wengi wenye nia na vipaji vya fani hiyo kuweza kujitangaza kitaifa na kimataifa.



MWISHO

Sunday, October 18, 2009

Nameless na Wahuu kufunika malipo ya ‘COSOTA’ ya Kenya



WANAMUZIKI wa Kenya wameanza kuneemeka kwa kupata faida ya kujiandikisha katika Chama cha Haki Miliki nchini humo (MCSK) kutokana na wengi wao kujiandikisha.

Akielezea hali hiyo mwenyekiti wa MCSK, Habel Kifoto alikiri kuwa kuna wanamuziki ambao wameshaanza kupata malipo yao kutokana na kujiandikisha kwenye utaratibu huo.

“Tutazunguka nchi nzima kuweza kutangaza umuhimu wetu na kila mwanamuziki au kikundi cha muziki kitatakiwa kuopata malipo yake kutoka katika kituo cha karibu pasipo kupata usumbufu wowote” alisema

Kwa mujibu wa habari zisizo thibitishwa Nameless na mkewe Wahu ni nyota wanaotarajiwa kupata mauzo makubwa zaidi.

MSHINDI WA BSS 2009!!!



Mshindi wa BSS, Cassian akipungia mashabiki mkono mara baada ya kutangazwa kutwaa kitita cha Shilingi Milioni 25 za kibongo, baada ya kukamua kisawasawa kwenye shoo hiyo, pembeni yake ni Mada Rita aliyemkabidhi mzigo huo.

JOHN JOSEPH HARAMBA NILIKUWEMO PIA



Mtu mzima na mimi nilikuwepo kususza macho nikiwa nimetinga t-shirt ya washkaji zangu 'WABISHI WA TAOWN' ila wananilipa mwana wanee oooh usifikiri navaa kuuza nyago tu.....pembeni yangu kulia na kushoto ni afanyakazi wenzangu.

ZITTO KABWE NDANI YA DIAMOND JUBELEE



Mizuka ilimpanda Mbunge wa Kigoma, Mh Zitto Kabwe katika ukumbi wa Diamond Jubelee na akaamua kuinuka kushangilia kama anavyoonekana, mambo yalikuwa sio mchezo ndani ya ukumbi huo.

BEATRICE NDANI YA DIAMOND JUBELEE



Mshiriki aliyeshina nafasi ya 5, Beatrice William akikamua jukwaani wimbo wa 'Chambua Kama Karanga' ndani ya Diamond Jubelee......

SHAA JUKWAANI



Mwanamuziki Sara Kaisi aka SHAA akiimba siku ya onyesho la BSS KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBELEE. Wanaoonekana kwa pembeni yake na nyuma ni dansers wake aliokuwa nao kutoka Tanzania House of Talent (THT)

CASSIAN AKIKAMUA JUKWAANI



Mshindin wa BSS, Paschal Casssian kutoka Mwanza akikamua jukwaani siku ya Shindano hilo katika ukumbi wa Diamond Jubelee

UNAMJUA HUYU!!!!!!!



Hivi ndivyo alivyokuwa miaka ya 1970, unamjua ni nani huyuuuuuuuu!!!!!

Anaitwa Ras Inno. Kwa ni mwanamuziki mkongwe wa Reggae wa hapa nchini ambaye kwa sasa licha ya kuendelea na kazi ya muziki pia ni mwandishi wa makala na kolam mbali mbali katika magazeti ya TANZANIA DAIMA na SAYARI.

RAS INNO, HIVI SASA



Ras Inno akiwa katika pozi katika picha iliyopigwa hivi karibuni.

RAS INNO JUKWAANI



Ras Inno akiimba jukwaani siku kumuezi Bob Marley mwaka 2003

RAS INNO NDANI YA MAWINGU



Ras Inno akiwa studio pande za Mawingu akifanya mambo.....

JAMANI WADAU MNAMKUMBUKA RAS INNO AKIWA NA JAKAYA!!!


Ras Inno, akipokea tuzo ya 2001 kutoka kwa Jakaya Kikwete aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje enzi hizo ambaye kwa sasa ndiye Presidaa wa Bongo. Katikati ni Hayati Mbamba. Kwa nyuma anayeonekana kwa mbali ni mmoja kati ya waimbaji a kundi la Unique Sister.

Picha kwa hisani ya Ras INNO mwenyewe.. Mzazi endelea kukamia kwa sana tunakuaminia....it me JOHN JOSEPH HARAMBA

Sunday, October 11, 2009

BSS KWENYE INTERVIEW



Mmoja kati ya washiriki wa BSS, Peter kiwa kwenye interview na mtangzaji mkongwe Godwin Gondwe zamani alijulikana kwa jina la Daouble G.

Sunday, September 27, 2009

HAPA AKIWA KATIKA POZI TOFAUTI

JAMANI MODO WETU HUYU, ANAKULA SHAVU STATE



NAME: JIMMY NGANYANGE
SUIT SIZE: 38
HEIGHT:
SHIRT:17
WAIST:34
ISEAM34
SHOE:12
BORN N RAISE: MOROGORO TANZANIA
CURRENT LOCATION: LOS ANGELOS CALIFORNIA

I ACTUALY GOT TWO DEAL WITH OTHER AGENCY CALLED YOUNG AGENCY MODELING I HAVE BEEN WITH THEM FOR ABOUT I JUST GOT INTO FORD NOT LONG AGO.SIMJUI MILLEN BADO MPYA KWENYE AGENCY PLUS FORD NI KUBWA ME NIPO FORD YA WEST COAST SHE MIGHT SOMEWHERE ELSE. BEEN MODELING ON N OFF FOR ABOUT 4YRS. LET ME KNOW IF U NEED MORE INFO BUT I SEND U 5 PHOTOS. GOD BLESS THX

Thursday, September 24, 2009

Fay kumsambaza shemeji



MWANADADA Faidha Omari ‘Sister Fay’ amekamilisha kurekodi video ya wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Shemeji’, utakaoanza sambazwa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni.

Kwa mujibu wa meneja wa msanii huyo Man Simba alisema mteja wake amepania kurejesha heshima ya jina lake kwenye fani hiyo baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu. “Kutokana na mambo kwenda kwa kasi tunatarajia kuanza kuisambaza video hiyo wiki ijayo” alisema Simba

Fay aliyewahi kuwa mwigizaji wa filamu kabla ya kujitosa kwenye muziki anafannya shughuli zake za kimuziki chini ya studio ya King J Records iliyopo Tabata Jijini.

'Utaipenda’ yawakutanisha Machozi na Joh Makini




HUSSEIN Machozi anayekamata kwenye medani ya muziki kupitia wimbo wa ‘Kwaajili Yako’, ameshirikiana na Joh Makini kutengeneza wimbo wa pili utakaofuatia kutoka kwenye vyombo vya habari, unaojulikana kwa jina la ‘Utaipenda’.

Kwa mujibu wa Meneja wa msanii huyo Sandu Mpanda ‘Kid Bway’ ambaye pia amekuwa akitayarisha nyimbo za Machozi kutoka studio ya Tetemesha Records iliyopo Mwanza alisema video ya wimbo wa ‘Utaipenda’ ipo kwenye hatua za mwisho, ukiwa umetengenezwa na Adam Juma wa kampuni ya Visual Lab.

Wimbo huo nao unapatika kwenye albamu ya ‘Kwa Ajili Yako’. Machozi aliwahi kutamba na nyombo za ‘Kafia Ghetto’, ‘Maji Yakimwagika’ na ‘Full Shangwe’.

Bifu ya Tunda Man na Spark yavunja filamu



KUFUATIA kuibuka kwa majibizano ya maneno ‘bifu’ kati ya wanamuziki Tunda Man na Spark walioimba wimbo wa ‘Nipe Ripoti’, hatma ya filamu yao iliyotokana kwa jina la ‘Nipe Ripoti’ haijulikani.

Filamu hiyo ilikuwa ijulikane kwa jina la ‘Nipe Ripoti’ iliyotokana na hadithi iliyokuwemo ndani ya wimbo huo, ilikuwa ikitengenezwa na kampuni ya video ya Kallage Pictures, ilisimama kutengenezwa kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Tunda Man na Spark waliokuwa wahusika wakuu kwa sasa hawaelewani mara baada ya Spark kujitoa kwenye kundi la Tip Top. Wahusika wote hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo isipokuwa Spark aliyesema filamu hiyo haipo tena.

Sunday, September 6, 2009

WANAMITINDO NJE YA NJENGO..PANDE ZA DODOMA



Wanamitindo na wabunufu wa mavazimaarufu wa hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya mjengo wa Bunge katika mji wa Dodoma, wabunifu hao walienda kwaajili ya kutembea na shughuli nyinginezo

HAPA AY HAPA JAY Z>>>>>



Mzee wa Biashara, AY akilonga na waandishi wa habari wakati wa kuelezea juu ya safari yao ya kwenye tuzo za MTV (MAMA) zitzkzofanyika Kenya. AY yupo kwenye kipengere kimoja na JAY Z.

Kipengere cha AY ni
Best Hip Hop
M.I. (Nigeria)
A.Y. (Tanzania)
Zulu Boy (South Africa)
Jay-Z (USA)
Kanye West (USA)

KWANINI SPARK KAJITOA TIP TOP!!!



Hatma ya kundi la Tip Top licha ya kunganisha nguvu na kundi la TMK Family inaonekana kutumba, kutokana na kuendelea kujitoa kwa wasanii katika kundi hilo. Baada ya kujitoa kwa MB Dog, kisha Z Anto na sasa Spark ametangaza kujitoa kwenye kundi hilo.
Swali linalobaki kichwani ni kwanini Spark amejitoa kwenye kundi hilo licha ya kuwa linaonekana kuwapa mafanikio wasanii wengi.

STOPA NA DJ TASS



Msanii wa Bongo Flava, Stopa akiwa ameweka pozi kwaajili ya picha pamoja na DJ Tass wa Radio Magic FM ya Jijini. Stopa ni kati ya wasanii watakao toa shoo ya nguvu kwenye ukumbi wa Dar West uliopo Tabata siku ya Idd Mosi.

Wasanii wegine ni Fid Q, Z Anto, Pingu na wengineo kibao

Sunday, August 30, 2009

MAMBO YA WARAKA HAYA !!!



Nyomi la wanadini wakitoa waraka wao katika viwanja vya Mnazimmoja

Sunday, August 2, 2009

MAPACHA WA HIP HOP WAJITOSA KWENYE MUVI



Wasanii wawili wa muziki wa Hip Hop nchini wanaojulikana kwa jina la ‘Mapacha’ Levison Kasulwa na James Kasulwa wameamua kujitosa katika uigizaji wa filamu kwa kile walichosema wanataka kujaribu maisha ya upande huo.

Mapacha waliotamba na nyimbo za ‘50 50’, ‘Jipe Moyo’ na ‘Sababu Ya Pesa’ wanatarajia kushiriki katika filamu inayojulikana kwa jina la ‘Sizya’ ambapo wao ndio waigizaji wakuu pamoja na mkongwe wa filamu nchini Lumele Matovolwa maarufu kwa jina la ‘Bigie’.

“Waandaaji wa filamu hiyo kampuni ya Chapakazi waliona tunafaa na wakaamua kutushirikisha katika filamu hiyo lakini haina maana tumeiweka kando iliyotupa umaarufu” alisema Levison

JOKATE AKIWA AMEPOZI



Hapa alikuwa amepozi akiwaangalia warembo walioshiriki kwenye Shindano la Miss Temeke 2009.

JOKATE KATIKA NGUO YENYE PICHA YA OBAMA

MAYA: BADO NIPO NIPO KWENYE FANI




Maya ni mmoja kati ya waigizaji aliyetamba mwanzoni mwa miaka ya 2000 katika michezo kadhaa ya televisheni iliyokuwa ikionyeshwa na kituo cha ITV ambayo iligizwa na kikundi cha Kaole Sanaa Group, amesema bado anaendeleza fani hiyo licha ya kutoonekana mara kwa mara katika vipindi hivyo.

“Nimeajiriwa kwenye kampuni ya Game 1st Quality inayojihusisha na masuala ya filamu, hivyo akili yangu yote ipo kwenye kuigiza filamu na sio maigizo ya kwenye televisheni.” Alifafanua Maya

Alisema ameamua kujibidiisha kwenye filamu kwakua zinalipa tofauti na maigizo ya kwenye televisheni, pia nia yake ni kujiendeleza kimataifa akidai Game 1st Quality wana malengo mazuri na wasanii wanaofanya nao kazi akimtolea mfano Kanumba kwa kusema kampuni hiyo imemsaidia kuonekana na kufika mbali.

ALLY CHOKI YUPO KENYA


Video za Extra Bongo kurekodiwa Kenya

Kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki yupo jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya kuandaa mazingira ya kurekodia video za nyimbo zao mpya.

Katika ziara hiyo Choki alisema yupo nchini humo kwaajili ya kuongea na kampuni itakayotumika kurekodi video hizo japo alisema ni mapema mno kutaja jina la kampuni hiyo na kuahidi ataweka wazi mara atakaporejea nchini.

Albamu ya Extra Bongo inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ikijulikana kwa jina la ‘Mjini Mipango’ ambao ni jina la moja ya wimbo unaopatikana ndani ya albamu hiyo ikiwa ni utunzi wa Choki mwenyewe.

NIMECHILL NA TWINS!!!



Mtu mzima John Joseph hpa nilikuwa na twins niliokutana nao anga flani za Msasani kwenye ofisi ya gazeti la Baab Kubwa. Majina yao sijui lakini nahisi mmoja anaitwa Kulwa na mwingine Doto, au ntakuwa nimekosea nini?

Sunday, July 26, 2009

DROGBA AHAMIA KWENYE KIKAPU




LaMarcus Aldridge (katikati) nyota wa mchezo wa kikapu wa timu ya Portland Trailblazers, akipozi kwa picha na wachezaji wa Chelsea FC, Didier Drogba (kulia) na Petr Cech mara baada ya kubadilishana jezi, juzi katika uwanja wa Cowboys jijini Texas kutakapofanyika mashindano ya nyota wa NBA.