
MMOJA kati ya wadau wa urembo nchini Taji Liundi ambaye anamiliki mtandao wa komputa wa modotz.blogspot.com, ameandaa shindano la kuwapata wanamitindo chipukizi mchakato utakaofanyika hivi karibuni na kujulikana kwa jina la Uniq Modo.
Akielezea mchakato huo alisema hawatozingatia kimo cha washiriki tofauti na dhana iliyopo kuwa mwanamitindo lazima awe mrefu. “Hata kwa wale ambao hawatabahatika kushinda, tutahakikisha inawajali kwa kuwatafutia kazi mbalimbali za uanamitindo kwa wale watakaoonyesha kuwa na nia ya kujiendeleza kwenye fani hiyo.” alisema
Alifafanua kuwa shindano la Uniq Modo ni mwanzo wa safari ndefu ambayo itafungua njia kwa vijana wengi wenye nia na vipaji vya fani hiyo kuweza kujitangaza kitaifa na kimataifa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment