Saturday, November 21, 2009

MWANAMBOKA KUWAONGOZA WENZAKE JUMAPILI HII



Na John Joseph

TAMASHA maalum la watoto linalojulikana kwa jina la Red Ribbon Children's Day linatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kesho kutwa kwa kushirikisha wanamitindo kadhaa maarufu wa hapa nchini.

Katika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House (TMH) Khadija Mwanamboka ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, alisema wabunifu hao wameamua kushiriki ili kutoa burudani kwa watoto ili kuwaonyesha jinsi wanavyowajali. Pia alisema watakuwepo wasanii wa muziki wa kiazazi kipya watakaosindikiza shughuli hiyo.

Wanamuziki hao ni Marlaw, Hemed, Profesa Jay, Mo Racka, Matonya, Chid Benz na Quick Rocka ambao watataoa burudani kwa watoto na wengineo watakaofika siku hiyo kushuhudia.

Aidha alitaja wanamitindo wengine watakaokuwepo siku hiyo na kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki ni Mustafa Hassanali, Ally Remtullah, Franko, Zamda George, Farha Sulatan na Asia Idarous atakaecheza ngoma ya kizanzibari itwayo ‘Bomu’.

Pia kutakuwa na mashindano ya kuimba na kucheza na zawadi nyingi zitatolewa kwa watoto. Sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo ni Clouds FM, Channel TEN, Entertainment Masters, Profesa Jay Foundation, Tanzania House of Talent (THT), Mokasi Medical System, Cool Blue na Shear Illusion.


MWISHO

No comments: