Sunday, October 18, 2009

Nameless na Wahuu kufunika malipo ya ‘COSOTA’ ya Kenya



WANAMUZIKI wa Kenya wameanza kuneemeka kwa kupata faida ya kujiandikisha katika Chama cha Haki Miliki nchini humo (MCSK) kutokana na wengi wao kujiandikisha.

Akielezea hali hiyo mwenyekiti wa MCSK, Habel Kifoto alikiri kuwa kuna wanamuziki ambao wameshaanza kupata malipo yao kutokana na kujiandikisha kwenye utaratibu huo.

“Tutazunguka nchi nzima kuweza kutangaza umuhimu wetu na kila mwanamuziki au kikundi cha muziki kitatakiwa kuopata malipo yake kutoka katika kituo cha karibu pasipo kupata usumbufu wowote” alisema

Kwa mujibu wa habari zisizo thibitishwa Nameless na mkewe Wahu ni nyota wanaotarajiwa kupata mauzo makubwa zaidi.

No comments: