MWANADADA Faidha Omari ‘Sister Fay’ amekamilisha kurekodi video ya wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Shemeji’, utakaoanza sambazwa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni.
Kwa mujibu wa meneja wa msanii huyo Man Simba alisema mteja wake amepania kurejesha heshima ya jina lake kwenye fani hiyo baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu. “Kutokana na mambo kwenda kwa kasi tunatarajia kuanza kuisambaza video hiyo wiki ijayo” alisema Simba
Fay aliyewahi kuwa mwigizaji wa filamu kabla ya kujitosa kwenye muziki anafannya shughuli zake za kimuziki chini ya studio ya King J Records iliyopo Tabata Jijini.
No comments:
Post a Comment