‘
HUSSEIN Machozi anayekamata kwenye medani ya muziki kupitia wimbo wa ‘Kwaajili Yako’, ameshirikiana na Joh Makini kutengeneza wimbo wa pili utakaofuatia kutoka kwenye vyombo vya habari, unaojulikana kwa jina la ‘Utaipenda’.
Kwa mujibu wa Meneja wa msanii huyo Sandu Mpanda ‘Kid Bway’ ambaye pia amekuwa akitayarisha nyimbo za Machozi kutoka studio ya Tetemesha Records iliyopo Mwanza alisema video ya wimbo wa ‘Utaipenda’ ipo kwenye hatua za mwisho, ukiwa umetengenezwa na Adam Juma wa kampuni ya Visual Lab.
Wimbo huo nao unapatika kwenye albamu ya ‘Kwa Ajili Yako’. Machozi aliwahi kutamba na nyombo za ‘Kafia Ghetto’, ‘Maji Yakimwagika’ na ‘Full Shangwe’.
No comments:
Post a Comment