Thursday, September 24, 2009

Bifu ya Tunda Man na Spark yavunja filamu



KUFUATIA kuibuka kwa majibizano ya maneno ‘bifu’ kati ya wanamuziki Tunda Man na Spark walioimba wimbo wa ‘Nipe Ripoti’, hatma ya filamu yao iliyotokana kwa jina la ‘Nipe Ripoti’ haijulikani.

Filamu hiyo ilikuwa ijulikane kwa jina la ‘Nipe Ripoti’ iliyotokana na hadithi iliyokuwemo ndani ya wimbo huo, ilikuwa ikitengenezwa na kampuni ya video ya Kallage Pictures, ilisimama kutengenezwa kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Tunda Man na Spark waliokuwa wahusika wakuu kwa sasa hawaelewani mara baada ya Spark kujitoa kwenye kundi la Tip Top. Wahusika wote hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo isipokuwa Spark aliyesema filamu hiyo haipo tena.

No comments: