
Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim ameondoka kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo ni mmoja kati ya washiriki wa shindano la Miss World 2008. Shindano litakalo fanyika katika mji wa Sun City tarehe 13 December 2008.
“Nimepewa maandalizi ya kutosha, nimefundishwa kutembea na mambo mengi ambayo yatanifanya nifanye vizuri”- Nasreen
Nasreen anakuwa mrembo wa 15 kushiriki mashindano hayo tangu mwaka 1994 yalipoanza tena. Nancy Sumari ndiye mwakilishi pekee kutoka Tanzania kufanya vizuri baada ya kutwa taji la Miss World Africa 2005.
Pichani Waziri wa mambo ya ndani Mh Laurence Masha ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi miss tanzania 2008 Nasreen Karim bendera ya uwakilishi.
No comments:
Post a Comment