Eti ni kweli kibongo bongo Hip Hop ilizaliwa pande za A-Town (Arusha)? Hiyondio imani ya rapa wa michano hiyo amabye pia ana talent ya uchoraji na utunzi wa vitabu Fred Tumaa aka Neno amabye ni dent wa Royal Collage akikamua Diploma in Journalism.
Albam anayo mkononi ila hawezi kwenda kichwa kichwa kwa wadosi si unawajua nao wale!!! Ikiwa na tracks kama vile “Kingdom” “Msalaba Na Kaburi”, “Sisomeki”, “Sauti Y Mtaani” na “Muda Umewadia” akiwa amewapa shavu wana kadhaa wakiwemo Blac, Mapacha, Kala, Shareef na Mansu Lee.
Dogo ametoka kwenye family ya Majeruhi ya Arusha. Mpaka sasa ameshatunga vitabu viwili ambavyo ni NO HOPE FOR TOMORROO na NYAYO YA MUUAJI
No comments:
Post a Comment