Baada ya ukimya wa muda mrefu comedian aliyesifika na kujipatia umaarufu kutokana na kuiga sauti za watu mashuhuri Steve Nyerere ameibuka na kuongea na John wa muzikimnene.
MN: Vipi mwana mbona kimya kingi kulikoni?
Steve: Du we acha tu nipo bwana nasongesha maisha kibongobongo, lakini zaidi najipanga kuja kufanya mambo mazuri zaidi sitaki kukurupuka yakaja kunitokea kama yaliyowatokea Komedi.
MN: Habari zilizopo mtaani ni kuwa huna jipya na ndio maana upo kimya.
Steve: Mimi ni mkongwe wa sanaa hii na ndiye msanii pekee ninayeongoza kwa kufanya shows nyingi ndani ya mjengo wa bunge. Nimefanya shows kwenye events kubwa nyingi sana leo hii ukiniambia nimeishiwa itakuwa vichekesho, natarajia kuanzisha stand up komedi ambayo hakuna mtu mwingine anayefanya Bongo nzima labda waibe idea yangu.
MN: Filamu yako ya “RESPECT OF NYERERE” ilipotelea wapi?
Steve: John sikiliza mimi nina hasira sana na hilo jambo mpaka sasa nina RL ya mwizi wangu wa filamu hiyo, ilini-cost hela nyingi sana mfano kumleta Teddy (video shooter) from Kenya kwa gharama zangu mwenyewe nikaitangaza mi mwenyewe kwa gharama kubwa, nashukuru wabunge walini changia kiasi. Nilipoenda kwa mdosi (DISRTIBUTER ) ananipa million 2, hivi huo si ni mchezo wa kuigiza!!! Hata cost ya kutengenezea haikutimia kwa mkwanja huo.
MN: So ulichukua uamuzi gani?
Steve: Niliamua kuiweka chini ya uvungu wa kitanda changu nitaiuza nikipata dau la kueleweka lakini sio hilo la wadosi. Lakini cha kustahajabisha ni kuwa VCD ya muvi hiyo ipo kitaani inauzwa, ilikotokaa sijui ila NIKIMKAMATA MWIZI WANGU WALAHI NITAM…..
1 comment:
Pole kaka ndo ukubwa huo. On the other side mansubiri nini kutumia wanataaluma kutunza haki zenu. Mko hai mnalizwa vipi mkivuta.... Mwaka 2009 hatutaki kusiki hizi stori tena!!
Post a Comment