Friday, November 7, 2008

MOTO WA MITIKISIKO WA PWANI




Haya! Haya! watu wa mipasho, baada ya kutikisa kwa miaka minne mwanadada tishio mjini Dida aka Khadija Shaibu akiwa sambamba na crew nzima ya TIME FM wanakuletea tamasha la kihistoria la kutimiza miaka minne ya kipindi cha “MITIKISIKO YA PWANI”. Katika kufanikisha tamasha hilo bendi zifuatazo zimealikwa:
Dar Modern Taarab
Jahazi Modern
TOP Taarab
New Zanzibar Star Coastal Modern
Tandale Modern & Super Shine

Bendi hizo zitapambanasiku ya tamasha ili kumjua nani mkali wa miondoko ya kimwambao, pia BASATA na wadau mbalimbali watahusishwa katika kuichagua bendi bora ya taarab wakiwemo washabiki na wasikilizaji wa TIMES FM watakao tuma sms katika kueleza chaguo lao.
‘Tamasha litafanyika tarehe 28 November 2008, wapi? Tutatangaza hivi karibuni. Unajua John mimi sitaki kubahatisha nataka liwe tamasha la kihistoria na ndio maana najipanga vizuri ili nikufunika kama ninavyofunika kwenye kipindi husika” alisema Dida

1 comment:

Anonymous said...

Taarabu imo? Tumeimeimisi sana mitikisiko. twataka jitikisia misumari kotekote. Tunasubiri kwa hamu kubwa