Wednesday, November 26, 2008

HELLO MUZIKIMNENE!!!!!




The gal anajulikana kwa jina la DYNA ni msanii wa kuimba akiwa anatokea pande za Dodoma, hapa alikuwa katika pose, kwa sasa anatamba na ngoma yake aliyompa shavu Marlaw. Kaa tayari kujua mengi kuhusu mrembo huyu kupitia hapahapa muzikimnene.blogspo.com

Tuesday, November 25, 2008

DR LOVE WA MAGIC FM & TIRA WA TRIPPLE A FM


Niky Ngonyani wa Magic FM akiwa anabadilishana mawazo na Tira Philip aka TIFEE pandee flani za Arusha siku ya uzinduzi wa Magic FM (98.6 FM)tarehe 15 November 2008 maeneo ya Masai Camp.

Monday, November 24, 2008

MACHINGA MPAKA KWENYE MAGODORO!!!




Vijana wa kitanzania wakiwa katika purukushani za kawaida za kimaisha, hapa wanaonekana vijana wawili waliokutwa na John wa muzikimnene wakiwa wanatembeza biashara ya magodoro maeneo ya Kipawa relini.

Friday, November 21, 2008

REVIEW YA OPRAH



OPRAH

WaigizajiI: Irene Uwoya 'Oprah',Ray ,Kanumba,Aunt
Mtunzi:Vicent Kigosi 'Ray'

Ray na Kanumba waliwahi soma wote shule ila walipotezana kwa muda mrefu hadi walipokutana tena Kijijini Ray akiwa mambo safi huko Kanumba akiwa choka mbaya,Ray akaamua kumsaidia Kanumba kwa kumchukua na kwenda ishi nae kwake ambako aliahidi mtibia kwania alikuwa anaumwa na kumsomesha ili aweze jiendeleza.

Oprah ambaye ni mke waRay hakupenda ujio wa Kanumba nyumbani kwake na alionyesha chuki za wazi wazi hadi siku yake ya kuzaliwa mabpo Kanumba alimzawadia zawadi ya ua na kuonyesha anamjali kuliko hata mumewe ndipo roho yake ilipomdondokea na kuanza kumtega kimapenzi ambapo kanumba nae alinasa.

Kama ujuavyo penzi ni kikohozi kulificha huwezi mapenzi yao yalikuwa yawazi yaliyopelekea mfanyakazi wa ndani kuyastukia na hadi Oprah kujua wameshajulikana na kuanza mfanyia visa ili aondoke ndani ya ile nyumba

Japo Ray alikuwa anapinga kuondoka kwake ila mwisho wasiku visa vilizidi kwani Opra alimuondosha kwa nguvu kwa kumchukua na kumsafirisha bila lumhirikisha Ray

Nae House Girl hakutaka ondoka hivi hivi alimpigia Ray siku na kumwekeza kuwa kuna barua amemuachia nyuma ya fremu ya picha ambayo ndo ina kisa cha yeye kuondolewa nadani yanyumba ile na mkewe Oprah

Ray alienda ifuata ile barua na alipofika ofisini aliifunga nakusoma ndo alipokuna barua ikieleza kigana ubaga mapenzi ya Oprah na Kanumba na kumuamuru mkewe asitoke nyumbani amsuri anarudi

STARS FANYENI MAMBO BWANA



Stars inabidi mwendeleze kukaza jabo hata tupate droo kwenye game linalokuja la marudiano ili tuwape watanzania raha, wajamani kwani sisi tunanini mpaka tuwe tunakosa kila siku utadhani tuna lala na bundi.
STAR TIMU KANDAMIZA SUDANI 4-0 TU ZINATOSHA WAENDE KWAO WAKAENDELEZE ,,hivi Sudani ni maarufu kwanini vile?????

NYOMI LA MAGIC FM






Nyomi la R-Chuga (Arusha) siku ya uzinduzi wa MAGIC FM huko kwenye mji wa baridi ambao zamani tulizoea kuuita half London.

Thursday, November 20, 2008

HAKUNA KUKATA TAMAA






Habari ndiyo hiyo mwanawane, hata katika maisha utakiwi kukata tamaa kwa kuogopa macho ya watu ilimradi unachokifanya ni sahihi katika jamii basi we zidisha kusonga.

Thanx to daddy wa Jacob Jr.

MAGIC FM IN A-CITY



Prodyuza Walter akiwa na Salma Msangi wote kutoka MAGIC FM wakiwa mitaa ya A-Town wakati wa tamasha la uzinduzi wa MAGIC FM pande za ARUSHA, Show ilikuwa kali ile yenyewe artistes kibao walikamua kutoka sides za Dar na Arusha kwenyewe.

Tuesday, November 18, 2008

VIPI SAFARI HII ATATUTOA KAMA NANCY?




Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim ameondoka kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo ni mmoja kati ya washiriki wa shindano la Miss World 2008. Shindano litakalo fanyika katika mji wa Sun City tarehe 13 December 2008.
“Nimepewa maandalizi ya kutosha, nimefundishwa kutembea na mambo mengi ambayo yatanifanya nifanye vizuri”- Nasreen
Nasreen anakuwa mrembo wa 15 kushiriki mashindano hayo tangu mwaka 1994 yalipoanza tena. Nancy Sumari ndiye mwakilishi pekee kutoka Tanzania kufanya vizuri baada ya kutwa taji la Miss World Africa 2005.

Pichani Waziri wa mambo ya ndani Mh Laurence Masha ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi miss tanzania 2008 Nasreen Karim bendera ya uwakilishi.

Tuesday, November 11, 2008

STEVE NYERERE AZURUMIWA




Baada ya ukimya wa muda mrefu comedian aliyesifika na kujipatia umaarufu kutokana na kuiga sauti za watu mashuhuri Steve Nyerere ameibuka na kuongea na John wa muzikimnene.

MN: Vipi mwana mbona kimya kingi kulikoni?
Steve: Du we acha tu nipo bwana nasongesha maisha kibongobongo, lakini zaidi najipanga kuja kufanya mambo mazuri zaidi sitaki kukurupuka yakaja kunitokea kama yaliyowatokea Komedi.
MN: Habari zilizopo mtaani ni kuwa huna jipya na ndio maana upo kimya.
Steve: Mimi ni mkongwe wa sanaa hii na ndiye msanii pekee ninayeongoza kwa kufanya shows nyingi ndani ya mjengo wa bunge. Nimefanya shows kwenye events kubwa nyingi sana leo hii ukiniambia nimeishiwa itakuwa vichekesho, natarajia kuanzisha stand up komedi ambayo hakuna mtu mwingine anayefanya Bongo nzima labda waibe idea yangu.
MN: Filamu yako ya “RESPECT OF NYERERE” ilipotelea wapi?
Steve: John sikiliza mimi nina hasira sana na hilo jambo mpaka sasa nina RL ya mwizi wangu wa filamu hiyo, ilini-cost hela nyingi sana mfano kumleta Teddy (video shooter) from Kenya kwa gharama zangu mwenyewe nikaitangaza mi mwenyewe kwa gharama kubwa, nashukuru wabunge walini changia kiasi. Nilipoenda kwa mdosi (DISRTIBUTER ) ananipa million 2, hivi huo si ni mchezo wa kuigiza!!! Hata cost ya kutengenezea haikutimia kwa mkwanja huo.
MN: So ulichukua uamuzi gani?
Steve: Niliamua kuiweka chini ya uvungu wa kitanda changu nitaiuza nikipata dau la kueleweka lakini sio hilo la wadosi. Lakini cha kustahajabisha ni kuwa VCD ya muvi hiyo ipo kitaani inauzwa, ilikotokaa sijui ila NIKIMKAMATA MWIZI WANGU WALAHI NITAM…..

Friday, November 7, 2008

MOTO WA MITIKISIKO WA PWANI




Haya! Haya! watu wa mipasho, baada ya kutikisa kwa miaka minne mwanadada tishio mjini Dida aka Khadija Shaibu akiwa sambamba na crew nzima ya TIME FM wanakuletea tamasha la kihistoria la kutimiza miaka minne ya kipindi cha “MITIKISIKO YA PWANI”. Katika kufanikisha tamasha hilo bendi zifuatazo zimealikwa:
Dar Modern Taarab
Jahazi Modern
TOP Taarab
New Zanzibar Star Coastal Modern
Tandale Modern & Super Shine

Bendi hizo zitapambanasiku ya tamasha ili kumjua nani mkali wa miondoko ya kimwambao, pia BASATA na wadau mbalimbali watahusishwa katika kuichagua bendi bora ya taarab wakiwemo washabiki na wasikilizaji wa TIMES FM watakao tuma sms katika kueleza chaguo lao.
‘Tamasha litafanyika tarehe 28 November 2008, wapi? Tutatangaza hivi karibuni. Unajua John mimi sitaki kubahatisha nataka liwe tamasha la kihistoria na ndio maana najipanga vizuri ili nikufunika kama ninavyofunika kwenye kipindi husika” alisema Dida

Thursday, November 6, 2008

ODEMBA OYEEE!!!




Mshiriki wa Tanzania Miriam Odemba akifurahi mara baada yakutangazwa mshindi wa pili wa mashindano ya Miss Earth yaliyofanyika mjini Manila, Phillipines juzi. Miss Phillipines Karla Henry kulia ndiye aliyeshinda taji hilo. Picha ya Reuters

MR ZEZE aka TID




Msanii wa bongo flava Khalid Mohamed akiwa anajiandaa kupanda kwenye karandina kurejea gerezani anakotumikia kifungo cha mwaka mmoja kutokana na makosa ya kumshabulia mtu mmoja kwenye ukumbi wa SLIP WAY jijini Dar es salaam.
Hapa alikuwa kitoka Mahakamani kukata rufaa dhidi ya hukumu yake hiyo.

ARUSHA ARE YOU READYYYYYY



For the first-tym ever in A-City wazee wa LIVE BILA ZENGWE aka MAGIC FM ya Dar es salaam siku ya Jumamosi tarehe 15 November 2008 Katika pande hizo watakuwa wakizindua frequency za MAGIC FM kupitia 98.6 FM, show ya nguvu itashushwa ndani ya viwanja vya Nane-Nane ……..Carnival
Katika kunogesha uzinduzi huo wa kihistoria wakazi wa Arusha watapolomoshewa burudani ya nguvu chini ya ma-DJ wa ukweli kutoka MAGIC FM pia wasanii wasio kuwa na idadi watawasha moto wakiwemo Dudu Baya, Nako 2 Nako, Watengwa, Stooper, Dully Sykes na wengine kibao cha kufurahisha zaidi ni kuwa mavituzi yote hayo yanatolewa FREEEEEEEE yaani BUREEEEE

Pichani ni Sam Misago (Prisenter) na DJ Tass wakiwa wamekula pose ndani ya studio za MAGIC FM

MULT TALENTED FROM A-CITY




Eti ni kweli kibongo bongo Hip Hop ilizaliwa pande za A-Town (Arusha)? Hiyondio imani ya rapa wa michano hiyo amabye pia ana talent ya uchoraji na utunzi wa vitabu Fred Tumaa aka Neno amabye ni dent wa Royal Collage akikamua Diploma in Journalism.
Albam anayo mkononi ila hawezi kwenda kichwa kichwa kwa wadosi si unawajua nao wale!!! Ikiwa na tracks kama vile “Kingdom” “Msalaba Na Kaburi”, “Sisomeki”, “Sauti Y Mtaani” na “Muda Umewadia” akiwa amewapa shavu wana kadhaa wakiwemo Blac, Mapacha, Kala, Shareef na Mansu Lee.
Dogo ametoka kwenye family ya Majeruhi ya Arusha. Mpaka sasa ameshatunga vitabu viwili ambavyo ni NO HOPE FOR TOMORROO na NYAYO YA MUUAJI

Wednesday, November 5, 2008

CHID BEENZ MUZIKI BASI TENA



Jamani ehee hivi ni kweli Chid Beenz kaamua kuutosa muziki?? mimi sisemi lakini habari ndio hiyo kiongozi huyo wa LA FAMILIA hataki tena kufanya muziki wa kibiashara labda eti awe anaimba na kusikiliza yeye mwenyewe ghetto kwake akiwa na washkaji zake...

Niambie mwana we unazungumziaje hii inshu....

HATARI!!!!!




Du wazee hii si ni hatyari sana hii,,hapa ni kituo cha Tabata Relini karibu na ofisi za MWANANCHI, gari la mizigo likiwa limeanguka katikati ya reli huku treni ya mizigo ikiwa inapita..Tumshukuru mungu ilikuwa katika speed ndogo.

MOSHI WA A-TOWN NOMA

Kuna washkaji watatu walikuwa wamechill kwenye chumba flani hivi wanapuliza kitu cha A-City aka Majani, basi bwana mjani ukiwa umekolea kibiriti walichokuwa wakikitumia kikawa kimeisha na still walikuwa wanakihitaji kukitumia ikabidi wamtume mwenzao mmoja kwenda kutafuta kibiriti, mchizi hakupinga ikabidi atoke nje kwenda kuatafuta kibiriti.
Mchizi alipofika nje akazunguka nje ya nyumba hilehile waliyokuwemo kisha akarudi kwa wale wale wana wake alipowakuta akaanza kusemesha huku akiwa anayumba yumba “Oya eehe machizi naombeni kiberiti kama kuna mtu anacho kati yenu?”
Wale wawili waliokuwa wamekaa wakamjibu “Kuna mwenetu mmoja ameenda kuazima hapo jirani kama vipi njoo tumsubiri atarudi muda sio mrefu”.

Tuesday, November 4, 2008



Hatimaye BABU ajitoa kundini,,msanii aliyekuwa akiwakilisha kundi la TMK WANAUME HALISI Babu aka Mtambo wa kurekebisha tabia kama anavyojiita yeye mwenyewe ameamua kujitoa kundini baada ya kuohakuna mafanikio aliyokuwa akipata na hakuna upendo wa kweli ndani ya kundi,,kwa hivi sasa Babu amesema kuwa atafanya kazi peke yake nila kuwa na kundi.

SNOOP MMMMM!!



Hivi huyu jamaa anazeeka lini eti kwa umri huu bado tu anapuliza.......@@#$$%%^^^

JIGGA & BEYONCE WAKIMSAPOTI OBAMA



Mtu mzima JIGGA alikuwa busy na mamaa BEYONCE katika kumpigia kampeni za mwisho mwisho Obama.

MABAGALA JAMANIIIII



Hivi lini adha hii iataisha jamani,,,hapa ni siku John wa muzikimnene alipoonja cha moto alipoenda kutembelea pande hizo, ilikuwa usipime huu ni mfano tu ebu chek...

RADO KUREJEA KWENYE GAME SOON


Unamkumbuka huyu jamaa???? Anaitwa Rado,,,mkali kutoka KIRAKA nadhani utakuwa umesha mrimemba alitamba sana kupitia ngoma ya “Usikulize”..Baada ya hapo akaachia ngoma moja nyingine kasha akaonekana kwenye kolabo kadhaa baada ya hapo akapotea,
Hapa alikuwa AIR PORT akiwa na mchizi wake wa KIRAKA kwenye mishe mishe zake za kawaida ndipo akakutana na John wa muzikimnene.

“Ebwana mi nipo mtu wangu sema skuli ndio imenibana sana si unajua nipo mwaka wa tatu ila usikonde soon mamabo yatakuwa fresh” alisema Rado

Stay tune kujua mengi kuhusu msela huyu kutoka MUZIKIMNENE

SAYANSI WA MATAJI



Huyu ni Sayansi moja kati ya memba wa Mataji Ya Miba, crew iliyosheheni vipaji vingi kamavile wanamuziki, waigizaji, wabunifu n.k Kwa sasa Sayansi amekamilisha albam yake akiwa solo na anarekebisha maswala flani ya promo kalba hajairelease rasmi.
Msanii huyu wa michano ya ki-hip hop amsha release single kadhaa zikiwemo “Harakati”, “Ombeni” na “Mapinduzi”. Memba wengine ni Snooza, Mabano, Rock, KwELI Kwanza, Mackvaigo na B.Charz.
“Pia tuna nguo zetu zenye chata la Mataji Ya Miba tunatarajia kuanza kuzisambaza soon tatizo bado tuna chek sponsor, kwa mawasiliano yoyote tunapatikana kwa namba 0713898782 na 0713114839” alisema Sayansi