Katika kusheherekea siku hiyo leo jioni, kituo cha kulea watoto yatima cha Tanzania Mitindo House kilichopo Magomeni wameandaa tafrija inayohusisha michezo mbalimbali , dikso na utoaji wa zawadi mbalimbali kwa watoto hao.
Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady JayDee’ atasheherekea siku yake ya kuzaliwa katika kituo hicho pia ataimba wimbo wa taifa pamoja na watoto hao.
Wageni waalikwa watakuwa ni watoto yatima kutoka vituo mbalimbali, wabunifu wa mavazi, watangazaji wa Radio na TV, wanamuziki, wanamitindo na warembo mbalimbali.
Taarifa hii ni kwamujibu wa mwanzilishi, Mwenyekiti na mlezi wa kituo hicho Khadija Mwanamboka
No comments:
Post a Comment