Wednesday, June 10, 2009

BOBI WINE AMPA KICHAPO BEBE COOL


Msanii Moses Ssali aka Bebe Cool, jumapili iliyopita alitumia muda wa takribani saa mbili akiwa hospitali baada ya kupata kichapo kutoka kwa msanii mwenzie wa nchi humo Robert Kyagulanyi aka Bobi Wine.
Wasanii hao ambao wamekuwa katika vita ya maneno kwa muda mrefu walikuwa katika ukumbi mmoja siku ya tukio kwenye uwanja wa Nakivubo stadium. Mchezo huo ulianza baada ya Bobi kusimama katika sehemu waliokuwemo kina Bebe Cool na mwenzake mara ghafla kukatokea majibizano ya maneno baina yao.
Bobi hakutaka kumchelewesha akaamua kumsukumizia makonde ya fasta fasta Bebe katika sehemu za tumboni na kifuani, katika kujihami Bebe akamsukuma Bobi nyuma.
Bebe alipelekwa hospitali ya Mayo, baada ya hapo alielekea katika kituo cha polisi cha Old Kampala kufungua kesi dhidi ya Bobi Wine.
Bobi hakupatikana kuzungumzia msala huo.

No comments: