
Msanii wa Uganda Bobi Wine ‘Rais wa Gheto’ yupo kwenye mazungumzo na mwanamuziki wa Ragga raia wa Jamaika, Buju Banton kutumbuiza katika tamasha la uzinduzi wa albamu yake hapo baadaye mwaka huu.
Vyanzo kutoka kundi la Bobi linalojulikana kwa jina la Fire Base Crew vimesema Bobi amemchagua Buju Banton kwasababu ni kati ya watu waliomvutia kuingia kwenye fani hii wakati anaanza muziki. Wakati huo huo kundi hilo pamoja na Bobi wameanza kutumbuiza kila wiki kwenye ukumbi wa Jam Session kwenye Baa ya Las Vegas maeneo ya Kabalagala na inasemekana kuwa huo ni upinzani kwa Jose Mayanja ‘Jose Chameleon’ anayetumbuiza kila jumatatu kwenye mghahawa wa Cherrie uliokaribu na eneo hilo.
No comments:
Post a Comment