Saturday, June 6, 2009

AKON HAUSIKI NA MIMBA YA MGANDA


Mwanamitindo raia wa Uganda, Susan Awori ilitaarifiwa kuwa anaujauzito ambao muhusika mkuu ni mwanamuziki msenegali anayeishi nchini Marekani Aliaune Thiam ‘Akon’.
Lakini kwa mujibu wa dada wa msichana huyo Sylvia Owori amekana kuwa Akon hausiki kwa chochote juu ya ujauzito huo. Maneno hayo yamekuja baada ya Akon kuonekana alikuwa karibu sana na binti huyo wakati alipotembelea nchini humo mwaka jana na kuonekana kuwa mtuwa karibu na Akon katika Hoteli ya Serena ambayo ndiyo aliyofikia.
“Kama angekuwa na ujauzito wa Akon hakika angekuwa ameshajifungua, hivyo tuache kuidanganya dunia hilo, muhusika wa ujauzito huo ni mwanamuziki wa hapahapa nyumbani (Uganda)” alisema Sylvia

No comments: