Saturday, June 13, 2009

MANSU LEE KUTOKA NA ALBAMU YA KINA KIREFU



Kina Kikirefu kumtoa Mansu Lee Mmoja kati ya wasanii wanachama wa kundi la KEPITO LETAZ Mansoor Ally
Mohamed 'Mansu Lee' amesema wimbo wimbo wake unaotamba kwa sasa unaojulikana kwa jina la Mengi Yanatokea aliutunga maalum kuelezea hisia zake dhidi ya mtayarishaji Hamis ‘Hermmy B’ aliyechukua tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Nyimbo mwaka huu kwenye tuzo za Kili.

“Hermy B na ndiye niliyeanza nae kipindi kile naanza muwika kwenye muziki na wimbo wa Kina Kirefu, baada ya muda alipata nafasi ya kufanya na wasanii wengine wenye majina hapo ndipo tulipoanza kutofautiana sababu kila nikimfata tufanye kazi ananiambia muziki hataki sababu haumlipi lakini baada ya muda nasikia kazi zake ambazo amezitengeneza yeye. Hali hiyo imeniuma na ndiyo maana nikatunga wimbo huo ili jamii ilelewe kinachoendelea”

Kuhusu kazi zake anasema albamu yake itajulikana kwa jina la Kina Kirefu itakuwa na nyimbo 14akiwashirikisha Josline, Ester Wasira, Squeezer na kundi lake la KAPITO LETAZ


imeandaliwa na john joseph haramba

No comments: