Tuesday, June 2, 2009

MZUNGU KUTOKA HOLLYWOOD AFANYA MAMBO BONGO



Huyu ndiye mzungu ambaye yupo Bongo kutoka HOLLYWOOD kule kwa kina Anord n.k akifanya mambo kwa kurekodi kazi kibao za wasanii wa kibongo. Kwa mujibu wa waandaaji wa project ya WAHAPAHAPA jamaa anaitwa JORDAN RIBER ametengeneza video za albamu ya mseto ya WAHAPAHAPA iliyotoka hivi karibuni na kuwashirikisha wasanii kibao kama vile LADY JAY DEE, BANANA ZORRO, ENIKA, FLORA MBASHA na wadau wengine kibao wakiwemo waigizaji na watayarishaji wa muziki kama vile JAY kutoka MAWINGU STUDIO.

SHOW ya bure itafanyika siku ya jumapili katika viwanja vya COCO BEACH,,,Kama vipi wana tujimix pande hizo au mnasemaje??

Mimi john Joseph wa muzikimnene.blogspot.com nitakuwemo pande hizo.

No comments: