Monday, June 29, 2009

RONALDO ATAPATA FURAHA KAMA HII TENA?



Ronaldo amekamilishataratibu za kuhamia Real Madrid kutoka Man U. lakini swali la kujiuliza atafanikiwa kuipata furaha kama hii aliyokuwa akiipata Man U.? hakika ni kusuburi na kungoja kitakachotokea.

BRAZIL OYEEEEE



Vijana wa kucheza samba, Brazili usiku wa jana wamewakandamiza vijana wa Obamakwa jumala ya mabao 3-2. Lakini katika hali ya kushangaza hadi kipindi cha pili kinamalizika Marekani walikuwa wakiongoza kwa bao 2-0.
Kweli wabrazil wa natisha.

THABIT AJIUNGA NBA



Mbongo mwezetu Hasheem Thabit amefanya kweli kwa kufanikiwa kuwa kati ya wachezaji walioijiunga katika ligi ya NBA huko pande flani za kina P.diddy. Mshkaji anastahili pongezi kwakua ameonyesha nia ya kujitumana mwisho wa siku amefanikiwa kufika juu.

Huu ni mfano wa kuigwa na sisi wabongo, tusifikiri kila kitu kinakuja easy lazima ukaze msuri. Hakuna kinachoshindikana jambo la muhimu ni kujua unapoelekea huku ukiwa na lanengo.

BIG UP THABIT KWA KUTUWAKILISHA VYEMA WABONGO

Tuesday, June 23, 2009

ALIKIBA KUKOLABO NA NYOTA WA MAREKANI



Alikiba inasemekana yupo kwenye mikakati ya kukolabo na Shari Watson aka Truth Hurts, wa Marekani.
Tega sikio kupata tarifa zaiidi kuhusu inshu hii soon.

MICHUZI JR AKIWA MZIGONI



Michuzi Jr akiwa mzigoni kama alivyonaswa na john joseph wa muzikimnene.blogspot.com

Saturday, June 13, 2009

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA LEO HII



Katika kusheherekea siku hiyo leo jioni, kituo cha kulea watoto yatima cha Tanzania Mitindo House kilichopo Magomeni wameandaa tafrija inayohusisha michezo mbalimbali , dikso na utoaji wa zawadi mbalimbali kwa watoto hao.

Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady JayDee’ atasheherekea siku yake ya kuzaliwa katika kituo hicho pia ataimba wimbo wa taifa pamoja na watoto hao.

Wageni waalikwa watakuwa ni watoto yatima kutoka vituo mbalimbali, wabunifu wa mavazi, watangazaji wa Radio na TV, wanamuziki, wanamitindo na warembo mbalimbali.

Taarifa hii ni kwamujibu wa mwanzilishi, Mwenyekiti na mlezi wa kituo hicho Khadija Mwanamboka

MMMMH HATA POZI ZA KULIA ZIPO ????



Mwanadada Thea akiwa kwenye moja ya pozi za kuli kwenye filamu ya DADAZ



Na John Joseph haramba....haramba29@yahoo.co.uk

DADAZ KUINGIA SOKONI HIVI KARIBUNI



Filamu ya kina dada inayoongozwa na Thea inatrajia kuingia sokoni hivi karibuni, katika filamu hiyo kila kitu kimewahusisha kina dada kwa kiasi kikubwa, kuanzia wahusika wakuu, wapiga picha n.k Thea ameahidi kuwa filamu hiyo itakuwa ni moja kati ya filamu kali za kibongo naimeonyesha kuwa kina dada wakipewa nafasi wanaweza kufanya.

Unaowaona kwenye picha ni kina dada watatu waliohusika kwa kiasi kikubwa kwenye filamu hiyo.

imeandaliwa na john joseph haramba
haramba29@yahoo.co.uk

JAY DEE NDANI YA MTANDAO



Judith Wambura aka Lady Jay Dee amefungua mtanao wake unaokwenda kwa jina la www.ladyjaydee.blogspot.com

MANSU LEE KUTOKA NA ALBAMU YA KINA KIREFU



Kina Kikirefu kumtoa Mansu Lee Mmoja kati ya wasanii wanachama wa kundi la KEPITO LETAZ Mansoor Ally
Mohamed 'Mansu Lee' amesema wimbo wimbo wake unaotamba kwa sasa unaojulikana kwa jina la Mengi Yanatokea aliutunga maalum kuelezea hisia zake dhidi ya mtayarishaji Hamis ‘Hermmy B’ aliyechukua tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Nyimbo mwaka huu kwenye tuzo za Kili.

“Hermy B na ndiye niliyeanza nae kipindi kile naanza muwika kwenye muziki na wimbo wa Kina Kirefu, baada ya muda alipata nafasi ya kufanya na wasanii wengine wenye majina hapo ndipo tulipoanza kutofautiana sababu kila nikimfata tufanye kazi ananiambia muziki hataki sababu haumlipi lakini baada ya muda nasikia kazi zake ambazo amezitengeneza yeye. Hali hiyo imeniuma na ndiyo maana nikatunga wimbo huo ili jamii ilelewe kinachoendelea”

Kuhusu kazi zake anasema albamu yake itajulikana kwa jina la Kina Kirefu itakuwa na nyimbo 14akiwashirikisha Josline, Ester Wasira, Squeezer na kundi lake la KAPITO LETAZ


imeandaliwa na john joseph haramba

Wednesday, June 10, 2009

BOBI WINE AMPA KICHAPO BEBE COOL


Msanii Moses Ssali aka Bebe Cool, jumapili iliyopita alitumia muda wa takribani saa mbili akiwa hospitali baada ya kupata kichapo kutoka kwa msanii mwenzie wa nchi humo Robert Kyagulanyi aka Bobi Wine.
Wasanii hao ambao wamekuwa katika vita ya maneno kwa muda mrefu walikuwa katika ukumbi mmoja siku ya tukio kwenye uwanja wa Nakivubo stadium. Mchezo huo ulianza baada ya Bobi kusimama katika sehemu waliokuwemo kina Bebe Cool na mwenzake mara ghafla kukatokea majibizano ya maneno baina yao.
Bobi hakutaka kumchelewesha akaamua kumsukumizia makonde ya fasta fasta Bebe katika sehemu za tumboni na kifuani, katika kujihami Bebe akamsukuma Bobi nyuma.
Bebe alipelekwa hospitali ya Mayo, baada ya hapo alielekea katika kituo cha polisi cha Old Kampala kufungua kesi dhidi ya Bobi Wine.
Bobi hakupatikana kuzungumzia msala huo.

Saturday, June 6, 2009

BINGWA WA NGUMI KWA KINADADA



Huyu ndiye bondia mwenye umri mdogo wa Tanzania ambaye ni bingwa wa mchezo huo kwa kina dada,,anaomba kama kuna mwenye uwezo amasaidie kufika mbali katika sanaa hiyo kwa sasa yupo chini ya JAPHET KASEBA akifanya mazoezi ya nguvu, binti anaitwa PENDO


john joseph haramba, haramba29@yahoo.co.uk

AKON HAUSIKI NA MIMBA YA MGANDA


Mwanamitindo raia wa Uganda, Susan Awori ilitaarifiwa kuwa anaujauzito ambao muhusika mkuu ni mwanamuziki msenegali anayeishi nchini Marekani Aliaune Thiam ‘Akon’.
Lakini kwa mujibu wa dada wa msichana huyo Sylvia Owori amekana kuwa Akon hausiki kwa chochote juu ya ujauzito huo. Maneno hayo yamekuja baada ya Akon kuonekana alikuwa karibu sana na binti huyo wakati alipotembelea nchini humo mwaka jana na kuonekana kuwa mtuwa karibu na Akon katika Hoteli ya Serena ambayo ndiyo aliyofikia.
“Kama angekuwa na ujauzito wa Akon hakika angekuwa ameshajifungua, hivyo tuache kuidanganya dunia hilo, muhusika wa ujauzito huo ni mwanamuziki wa hapahapa nyumbani (Uganda)” alisema Sylvia

BUJU BANTONI KUTUA UGANDA


Msanii wa Uganda Bobi Wine ‘Rais wa Gheto’ yupo kwenye mazungumzo na mwanamuziki wa Ragga raia wa Jamaika, Buju Banton kutumbuiza katika tamasha la uzinduzi wa albamu yake hapo baadaye mwaka huu.

Vyanzo kutoka kundi la Bobi linalojulikana kwa jina la Fire Base Crew vimesema Bobi amemchagua Buju Banton kwasababu ni kati ya watu waliomvutia kuingia kwenye fani hii wakati anaanza muziki. Wakati huo huo kundi hilo pamoja na Bobi wameanza kutumbuiza kila wiki kwenye ukumbi wa Jam Session kwenye Baa ya Las Vegas maeneo ya Kabalagala na inasemekana kuwa huo ni upinzani kwa Jose Mayanja ‘Jose Chameleon’ anayetumbuiza kila jumatatu kwenye mghahawa wa Cherrie uliokaribu na eneo hilo.

Tuesday, June 2, 2009

VIMWANA WA MISS MZIZIMA 2009



Warembo wanaotarajia kuchuana katika kinyang'anyiro cha kumsaka MISS MZIZIMA 2009 mwishoni mwa wiki hii wakiwa wamepozi kwaajili ya picha mara baada ya kutembelwa na wanahabari nikiwemo mimi JOHN JOSEPH wa muzikimnene.blogspot.com

BANANA ZORRO AKICHONGA KUHUSU WAHAPAHAPA



Mmoja kati ya wanamuziki watakao tumbuiza kwenye tamasha la WAHAPAHAPA ambaye pia ameshiriki katika albamu hiyo kwa kuimba wimbo wa ZOBA, sio mwingine ni BANANA ZORRO akisisitiza jambo wakati akizungumza za waandishi wa gabari.

MZUNGU KUTOKA HOLLYWOOD AFANYA MAMBO BONGO



Huyu ndiye mzungu ambaye yupo Bongo kutoka HOLLYWOOD kule kwa kina Anord n.k akifanya mambo kwa kurekodi kazi kibao za wasanii wa kibongo. Kwa mujibu wa waandaaji wa project ya WAHAPAHAPA jamaa anaitwa JORDAN RIBER ametengeneza video za albamu ya mseto ya WAHAPAHAPA iliyotoka hivi karibuni na kuwashirikisha wasanii kibao kama vile LADY JAY DEE, BANANA ZORRO, ENIKA, FLORA MBASHA na wadau wengine kibao wakiwemo waigizaji na watayarishaji wa muziki kama vile JAY kutoka MAWINGU STUDIO.

SHOW ya bure itafanyika siku ya jumapili katika viwanja vya COCO BEACH,,,Kama vipi wana tujimix pande hizo au mnasemaje??

Mimi john Joseph wa muzikimnene.blogspot.com nitakuwemo pande hizo.

MR PAUL KWELI KUREJEA KWENYE GAME ????



Kuna tetesi kuwa mtu mzima Mr Paul aliyewahi kutamba miaka ya mwanzoni mwa 2000 kupitia nyimbo kama vile ZUWENA, GOZIGOZI na nyinginezo nyingi ambazo kwa wale wafuatiliaji watakuwa wanazifahamu inadaiwa mshkaji anmpango wa kurejea kwenye game la muziki baada ya kimya cha muda mrefu.