Mshiriki wa shindano la Miss Tanzania 2003, Leyla Bahji aliyefanikiwa kufika kumi bora ya mashindano kwa mwaka huo amesema sanaa ya urembo imeanza kurejesha umaarufu wake uliopotea kutokana na tabia zisizopendeza mbele ya jamii zilizofanywa na baadhi ya washiriki waliopitia kwenye kinyanganyiro hicho.
Pia Leyla aliyekuwa ni mwanamitindo kwa sasa ni mmoja kati ya waandaaji wa Miss Ilala ameongeza kwa kusema kuwa japo kwa sasa ameolewa lakini anajushughulisha kuwafundisha warembo mambo mbalimbali. “Sanaa ya urembo nimeisomea nchini India hivyo ninaijua vizuri, kati ya vitu ninavyowafundisha warembo ni kuwa na nidhamu, kujibu maswali n.k” alisema mrembo huyu ambaye pia ni mfanyakazi wa TPA.
No comments:
Post a Comment