Friday, May 15, 2009

TunakuJa na video kali ya mwaka



KUNDI la TMK Unit linaloongozwa na wasanii sita ambao ni UB, BMC, Dula B, Sir G, Nemy na Dogo Ally waliotesa na video ya wimbo wao wa Haitoshi wanatarajia kuibuka na video yao ya pili itakayojulika kwa jina la Kaburi La Dunia.
Akuzungumzia suala hilo, meneja wa kundi hilo, Ashiraf Musa alisema:
‘Video hiyo inarekodiwa na kampuni ya Brayance Production itakuwa kali kuliko video nyingi za kibongo na ni kati ya kazi zetu zilizomo kwenye albamu,” alisema na kuongeza:
‘Mpaka sasa kuna baadhi ya vipande vya video hiyo vimeshakamilika vikiwa vimerekodiwa katika sehemu mbalimbali za jiji chini ya uiongozi wa Hassan Mbangwa na mimi mwenyewe” alisema Shira.

No comments: