
MTANGAZAJI mkongwe Kareem Omari aka ‘K.O’ anayetangaza kwenye kituo cha redio cha Kifimbo FM kilichopo Dodoma amewashauri wasanii wa kujitanua zaidi mikoani kuliko kufanya Dar ndio kila kitu.
Kabla ya kutua katika kituo hicho K.O alikuwa ni mtangazaji wa Times FM ya Dar es salaam anasema “Tangu nilipokuja huku watu wamenikubali ila kiasi fulani nakuwa nachelewa kupata nyimbo na baadhi ya taarifa za wasanii maarufu kutokana na wao kuto jitanua na kujitangaza mikoani”
“Kama msanii anashindwa kuwawezesha watu wa Dodoma kujua habari zake inakuwa ngumu kwake kuwajulisha walio nje ya nchi” alisema K.O ambaye ndiye msimamizi wa vipindi katika kituo hicho.
Kwenye picha K.O ni wakatikati aliye unama akiwa na machizi kibao akiwemo tu mzima Afande Sele.
INTERVIEW HII PIA INAPATAKINA KWENYE GAZETI LA TANZANIA DAIMA LA 15 MAY 2009 UKURASA WA 20.
No comments:
Post a Comment