Thursday, May 21, 2009

SUMA G ATESA NA HAWAKAI



RAPA wa kundi la Hot Pot Family, Ismail Seif ‘Suma G’ aliyepata kuwika kwa wimbo wa “Vituko Uswahilini” amerejea dimbani na wimbo mpya wa ‘Hawakai’ aliomshirikisha prodyuza Mako Chali wa MJ Records.
Suma anadai, baada ya kudhurumiwa mauzo ya albamu yake ya pili ya iliyojulikana kwa jina la Aibu Yao, kwa sasa ameamua kujipanga mpya.
‘Albam ‘u hile’ iliingia sokoni bila ridhaa yangu pasipo kutangazwa hata kidogo hali iliyosababisha atoke kapa ili kuepusha migongano kati yangu na wadau walionisimamia kazi hiyo, nimeamua kuachana nayo japo ni haki kudai jasho langu. Nimeamua kuelekeza nguvu katika albam yangu ijayo ambayo kama mipango ikienda vizuri itakuwa tayari mwezi Juni.” alisema Suma G.

No comments: