Friday, May 15, 2009

NAJIANDAA KUONGEZA UJUZI ULAYA



Mwigizaji Issa Musa Hamis ‘Cloud’ aliyejipatia umaarufu kutokana na kuigiza katika tamthilia za televisheni kisha akahamia kwenye filamu, sasa ameongeza ujuzi mwingine wa uhariri na upigaji picha wa filamu.
“Nia yangu ni kufika mbali zaidi ya hapa nilipo na nimeshaanza mipango ya kwenda kusoma nje nikianzia katika chuo flani kilichopo Nairobi baada ya hapo nitaelekea kwenye moja ya nchi zilizo bara la Ulaya” alisema Cloud ambaye ni mfanya kazi wa Sofia Production.
Baadhi ya filamu alizoziongoza ni Valentine, Mid Night, Silent Killer, Mchanga Wa Macho na Kaburi La Mapenzi. Cloud amesema yupo tayari kukosolewa pindi anapokosea lakini isiwe kisingizio cha kumkashifu kwa yale anayoyafanya.

No comments: