
Kundi la Watu Wa Gola wanatarajia kufanya onyesho kwaajili ya utambulisho wa wimbo wao mpya wa Maria na video yao ya Mtoto Ya Gola katika ukumbi wa New Generation uliopo Igoma jumatano ijayo.
Akizungumza na SAYARI meneja wa kundi hilo Linda Sagudi kazi hizo ni kati ya zitakazokuwemo kwenye albam yao ya Vichwa Vya Kale itakayozinduliwa Disemba mwaka huu. Watunzi wa nyimbo zitakazo kuwemo kwenye albamu hiyo ni Juma Hasani 'Big D', Paskal linda 'Batarokota', C-Rob na Daz P.
Onyesho hilo limedhaminiwa na kituo cha kusaidia watoto yatima na wajane (Huruma Children Centre), Stream ii Co. Ltd, G-Unit Music and Commucation, Masese Grocery na Nyuki Grocery. Baada ya utambulisho huo burudani ya muziki itashushwa kutoka kwa Dj Zari, Dj Casto, Dj Peter na Dj Opio huku wasanii waalikwa watakuwa Daz P, Y Bring bring, Mchomoko.
No comments:
Post a Comment