Sunday, May 31, 2009

SIFA YA UREMBO INAREJE



Mshiriki wa shindano la Miss Tanzania 2003, Leyla Bahji aliyefanikiwa kufika kumi bora ya mashindano kwa mwaka huo amesema sanaa ya urembo imeanza kurejesha umaarufu wake uliopotea kutokana na tabia zisizopendeza mbele ya jamii zilizofanywa na baadhi ya washiriki waliopitia kwenye kinyanganyiro hicho.
Pia Leyla aliyekuwa ni mwanamitindo kwa sasa ni mmoja kati ya waandaaji wa Miss Ilala ameongeza kwa kusema kuwa japo kwa sasa ameolewa lakini anajushughulisha kuwafundisha warembo mambo mbalimbali. “Sanaa ya urembo nimeisomea nchini India hivyo ninaijua vizuri, kati ya vitu ninavyowafundisha warembo ni kuwa na nidhamu, kujibu maswali n.k” alisema mrembo huyu ambaye pia ni mfanyakazi wa TPA.

HAWA NI BINADAMU KWELI??????



Vijana wenye vipaji vya acrobatic wakonyesha ujuzi wao jukwaani kwenye onyesho la mavazi lililoandaliwa na Ally kwenye ukumbi wa Movenpick last wiki. Vijana hawa waliteka stage kiasi cha kuwaacha watu wakiwashangaa wao!!!!

REHMTULAH ON THE STAGE



Mbunifu mwenyewe Ally Rehmtulah akikatisha jukwaani mara baada ya wanamitindo kupita kuonyesha mavazi yake, Hapa alikuwa na full tabasamu. Show ilikuwa nzuri kama jinsi nilivyoishuhudia mimimwenyewe JOHN JOSEPH wa muzikimnene.blogspot.com

MREMBO JUKWAANI



Moja kati ya warembo akikatisha on the stage wakati wa onyesho la mavazi lililoandaliwa na Ally Rehmtulah @ Movenpick wiki iliyopita.

Thursday, May 21, 2009

SUMA G ATESA NA HAWAKAI



RAPA wa kundi la Hot Pot Family, Ismail Seif ‘Suma G’ aliyepata kuwika kwa wimbo wa “Vituko Uswahilini” amerejea dimbani na wimbo mpya wa ‘Hawakai’ aliomshirikisha prodyuza Mako Chali wa MJ Records.
Suma anadai, baada ya kudhurumiwa mauzo ya albamu yake ya pili ya iliyojulikana kwa jina la Aibu Yao, kwa sasa ameamua kujipanga mpya.
‘Albam ‘u hile’ iliingia sokoni bila ridhaa yangu pasipo kutangazwa hata kidogo hali iliyosababisha atoke kapa ili kuepusha migongano kati yangu na wadau walionisimamia kazi hiyo, nimeamua kuachana nayo japo ni haki kudai jasho langu. Nimeamua kuelekeza nguvu katika albam yangu ijayo ambayo kama mipango ikienda vizuri itakuwa tayari mwezi Juni.” alisema Suma G.

BATAROKOTA KUTOKA MWANZA



Kundi la Watu Wa Gola wanatarajia kufanya onyesho kwaajili ya utambulisho wa wimbo wao mpya wa Maria na video yao ya Mtoto Ya Gola katika ukumbi wa New Generation uliopo Igoma jumatano ijayo.

Akizungumza na SAYARI meneja wa kundi hilo Linda Sagudi kazi hizo ni kati ya zitakazokuwemo kwenye albam yao ya Vichwa Vya Kale itakayozinduliwa Disemba mwaka huu. Watunzi wa nyimbo zitakazo kuwemo kwenye albamu hiyo ni Juma Hasani 'Big D', Paskal linda 'Batarokota', C-Rob na Daz P.

Onyesho hilo limedhaminiwa na kituo cha kusaidia watoto yatima na wajane (Huruma Children Centre), Stream ii Co. Ltd, G-Unit Music and Commucation, Masese Grocery na Nyuki Grocery. Baada ya utambulisho huo burudani ya muziki itashushwa kutoka kwa Dj Zari, Dj Casto, Dj Peter na Dj Opio huku wasanii waalikwa watakuwa Daz P, Y Bring bring, Mchomoko.

Friday, May 15, 2009

NAJIANDAA KUONGEZA UJUZI ULAYA



Mwigizaji Issa Musa Hamis ‘Cloud’ aliyejipatia umaarufu kutokana na kuigiza katika tamthilia za televisheni kisha akahamia kwenye filamu, sasa ameongeza ujuzi mwingine wa uhariri na upigaji picha wa filamu.
“Nia yangu ni kufika mbali zaidi ya hapa nilipo na nimeshaanza mipango ya kwenda kusoma nje nikianzia katika chuo flani kilichopo Nairobi baada ya hapo nitaelekea kwenye moja ya nchi zilizo bara la Ulaya” alisema Cloud ambaye ni mfanya kazi wa Sofia Production.
Baadhi ya filamu alizoziongoza ni Valentine, Mid Night, Silent Killer, Mchanga Wa Macho na Kaburi La Mapenzi. Cloud amesema yupo tayari kukosolewa pindi anapokosea lakini isiwe kisingizio cha kumkashifu kwa yale anayoyafanya.

JOHN JOSEPH - OWNER WA MUZIKIMNENE.BLOGSPOT.COM




Mwanashavu jipe mwenyewe ukingoja kungojea sometimes unaweza usilipate, mtu mzima hapo nilikuwa ndani ya Kempiski nikipata moja baridi moja moto.

Kama una coments zozote chek nami kwenye mail yangu: haramba29@yahoo.co.uk

Big up kwa wanangu wote wa mikoani kwa kunipa sapoti TUKO PAMOKO SAAANA

VIOLET AENDA U.S.A



kwaajili ya kupumzika na kuangalia mustakabali mwingine wa maisha yake ya mbeleni.
Akiongea na SAYARI muda mfupi kabla ya kuondoka msanii huyo aliyetamba kwenye filamu za Super Model, Ukungu, Segito, Binti Nusa, The Sins Of My Father na Sikitiko Langu alisema ameamua kuelekea katika nchi hiyo iliyo bara la Amerika baada ya kuitwa na mjoamba wake.
“Kuna matatizo fulani yalijitokeza hivi karibuni najua nikifika huko nitakuwa na muda mzuri wa kupumzika kisha badaya muda ndiyo nitajua nini cha kufanya” alisema Violet

TunakuJa na video kali ya mwaka



KUNDI la TMK Unit linaloongozwa na wasanii sita ambao ni UB, BMC, Dula B, Sir G, Nemy na Dogo Ally waliotesa na video ya wimbo wao wa Haitoshi wanatarajia kuibuka na video yao ya pili itakayojulika kwa jina la Kaburi La Dunia.
Akuzungumzia suala hilo, meneja wa kundi hilo, Ashiraf Musa alisema:
‘Video hiyo inarekodiwa na kampuni ya Brayance Production itakuwa kali kuliko video nyingi za kibongo na ni kati ya kazi zetu zilizomo kwenye albamu,” alisema na kuongeza:
‘Mpaka sasa kuna baadhi ya vipande vya video hiyo vimeshakamilika vikiwa vimerekodiwa katika sehemu mbalimbali za jiji chini ya uiongozi wa Hassan Mbangwa na mimi mwenyewe” alisema Shira.

MUNGU YUKO BIZE, KWENYE VIDEO



Bwana Misosi hivi sasa yupo mzigoni akishuti video ya Mungu Yuko busy chini ya kampuni ya Visual Lab. Mshkaji amesema anamini video hiyo itakuwa ya ukweli na anaamini itamsudishia heshima yake iliyopotea kwa kipindi kirefu kama jinsi ambavyo wimbo huo unavyotesa kwenye vituo vya redio,

Thursday, May 14, 2009

Wasanii jitangazeni mikoani - k 2 da.........




MTANGAZAJI mkongwe Kareem Omari aka ‘K.O’ anayetangaza kwenye kituo cha redio cha Kifimbo FM kilichopo Dodoma amewashauri wasanii wa kujitanua zaidi mikoani kuliko kufanya Dar ndio kila kitu.

Kabla ya kutua katika kituo hicho K.O alikuwa ni mtangazaji wa Times FM ya Dar es salaam anasema “Tangu nilipokuja huku watu wamenikubali ila kiasi fulani nakuwa nachelewa kupata nyimbo na baadhi ya taarifa za wasanii maarufu kutokana na wao kuto jitanua na kujitangaza mikoani”

“Kama msanii anashindwa kuwawezesha watu wa Dodoma kujua habari zake inakuwa ngumu kwake kuwajulisha walio nje ya nchi” alisema K.O ambaye ndiye msimamizi wa vipindi katika kituo hicho.

Kwenye picha K.O ni wakatikati aliye unama akiwa na machizi kibao akiwemo tu mzima Afande Sele.

INTERVIEW HII PIA INAPATAKINA KWENYE GAZETI LA TANZANIA DAIMA LA 15 MAY 2009 UKURASA WA 20.

Saturday, May 2, 2009

PROFESA JAY KUPIGA KOLABO NA MGHANA




Joseph Haule ‘Profesa Jay’ amerekodi wimbo mmoja na Kwa Kwese ambaye ni msanii wa Ghana, wimbo unaitwa Who We Be. Video ya wimbo hiyo inasemekana ipo jikoni na inatengenezwa kwa ushirikiano wa MTV Base.

ROCK CITY



Haya mawe yanaitwa Bismack, yapo pande za Mwanza. Mtumzima huko ndiko mtu mzima John Joseph niliko zaliwa na kukulia kabla sijatimba maguu mitaa flani ya town.

NGASA APAJA JIKO



Mchezaji wa timu ya DAR ES SALAAM YOUNG AFRICAN (YANGA) Mrisho Ngasa akiwa na mkewe mara baada ya kufunga naye pingu za maisha huko Tabata.