Sunday, September 27, 2009
JAMANI MODO WETU HUYU, ANAKULA SHAVU STATE
NAME: JIMMY NGANYANGE
SUIT SIZE: 38
HEIGHT:
SHIRT:17
WAIST:34
ISEAM34
SHOE:12
BORN N RAISE: MOROGORO TANZANIA
CURRENT LOCATION: LOS ANGELOS CALIFORNIA
I ACTUALY GOT TWO DEAL WITH OTHER AGENCY CALLED YOUNG AGENCY MODELING I HAVE BEEN WITH THEM FOR ABOUT I JUST GOT INTO FORD NOT LONG AGO.SIMJUI MILLEN BADO MPYA KWENYE AGENCY PLUS FORD NI KUBWA ME NIPO FORD YA WEST COAST SHE MIGHT SOMEWHERE ELSE. BEEN MODELING ON N OFF FOR ABOUT 4YRS. LET ME KNOW IF U NEED MORE INFO BUT I SEND U 5 PHOTOS. GOD BLESS THX
Thursday, September 24, 2009
Fay kumsambaza shemeji
MWANADADA Faidha Omari ‘Sister Fay’ amekamilisha kurekodi video ya wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Shemeji’, utakaoanza sambazwa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni.
Kwa mujibu wa meneja wa msanii huyo Man Simba alisema mteja wake amepania kurejesha heshima ya jina lake kwenye fani hiyo baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu. “Kutokana na mambo kwenda kwa kasi tunatarajia kuanza kuisambaza video hiyo wiki ijayo” alisema Simba
Fay aliyewahi kuwa mwigizaji wa filamu kabla ya kujitosa kwenye muziki anafannya shughuli zake za kimuziki chini ya studio ya King J Records iliyopo Tabata Jijini.
'Utaipenda’ yawakutanisha Machozi na Joh Makini
‘
HUSSEIN Machozi anayekamata kwenye medani ya muziki kupitia wimbo wa ‘Kwaajili Yako’, ameshirikiana na Joh Makini kutengeneza wimbo wa pili utakaofuatia kutoka kwenye vyombo vya habari, unaojulikana kwa jina la ‘Utaipenda’.
Kwa mujibu wa Meneja wa msanii huyo Sandu Mpanda ‘Kid Bway’ ambaye pia amekuwa akitayarisha nyimbo za Machozi kutoka studio ya Tetemesha Records iliyopo Mwanza alisema video ya wimbo wa ‘Utaipenda’ ipo kwenye hatua za mwisho, ukiwa umetengenezwa na Adam Juma wa kampuni ya Visual Lab.
Wimbo huo nao unapatika kwenye albamu ya ‘Kwa Ajili Yako’. Machozi aliwahi kutamba na nyombo za ‘Kafia Ghetto’, ‘Maji Yakimwagika’ na ‘Full Shangwe’.
Bifu ya Tunda Man na Spark yavunja filamu

KUFUATIA kuibuka kwa majibizano ya maneno ‘bifu’ kati ya wanamuziki Tunda Man na Spark walioimba wimbo wa ‘Nipe Ripoti’, hatma ya filamu yao iliyotokana kwa jina la ‘Nipe Ripoti’ haijulikani.
Filamu hiyo ilikuwa ijulikane kwa jina la ‘Nipe Ripoti’ iliyotokana na hadithi iliyokuwemo ndani ya wimbo huo, ilikuwa ikitengenezwa na kampuni ya video ya Kallage Pictures, ilisimama kutengenezwa kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.
Tunda Man na Spark waliokuwa wahusika wakuu kwa sasa hawaelewani mara baada ya Spark kujitoa kwenye kundi la Tip Top. Wahusika wote hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo isipokuwa Spark aliyesema filamu hiyo haipo tena.
Sunday, September 6, 2009
WANAMITINDO NJE YA NJENGO..PANDE ZA DODOMA
HAPA AY HAPA JAY Z>>>>>
KWANINI SPARK KAJITOA TIP TOP!!!

Hatma ya kundi la Tip Top licha ya kunganisha nguvu na kundi la TMK Family inaonekana kutumba, kutokana na kuendelea kujitoa kwa wasanii katika kundi hilo. Baada ya kujitoa kwa MB Dog, kisha Z Anto na sasa Spark ametangaza kujitoa kwenye kundi hilo.
Swali linalobaki kichwani ni kwanini Spark amejitoa kwenye kundi hilo licha ya kuwa linaonekana kuwapa mafanikio wasanii wengi.
STOPA NA DJ TASS
Subscribe to:
Posts (Atom)