Wednesday, March 18, 2009

ZOLA D APATA TUZO NCHINI KENYA




Baada ya kuona muziki wa Bongo ukimzingua pasipo kupata mafanikio ya anavyotaka msanii wa kufoka foka wa kitanzania Zola D ameamua kuhamishia kazi zake nje ya mipaka ya Tanzania kwa kutafuta soko la nje na kwakuanzia anasema kuwa amepata tuzo kwenye tuzo zinazojulikana kwa jina la Coastal Music Awards (KE) kupitia wimbo wake wa "Hoi" aliyofanya pamoja na Cannibal wa Kenya.

"Bongo nimeona sifanikiwi kivile na ndio maana nimeona bora nielekeze nguvu zangu nje ambako nathaminiwa zaidi kuliko hapa nyumbani, mpaka sasa nimeshatengeneza kazi zaidi ya nane na Cannibal. Na katika kutanua wigo zaidi natarajia kufungua kituo changu cha radio katika nji wa Moshi. kwasasa nina safari ya kuelekeea bara la Ulaya kwanza kisha nikirudi ndio nakamilisha mambo yote yaliyobaki" alinena Zola D

No comments: