Mcheza show mkongwe wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Hassan Mohamed maarufu kwa jina la Super Nyamwela, amesema baada ya albamu yake ya kwanza aliyoitengeneza nje ya bendi yake kupata mafanikio katika soko la muziki. Anatarajia kuachia albamu yake ya pili ambayo mpaka sasa bado hajajua itaitwaje.
Akizungumzia habari hizo Nyamwela anasema amepanga mpaka kufikia mwezi Aprili mwaka huu awe amekamilisha albamu itakayokuwa na nyimbo sita na kuingia sokoni. “Master On The Temple” ndio jina la albamu yake ya kwanza. Nyamwela amedumu kwenye bendi ya Twanga Pepeta tangu mwaka 2000 akitokea kundi la Billi Bums lililokuwa likifanya show kwenye ukumbi wa Billicanas.
“Sijajua niipe jina gani mpaka sasa ila itakuwa na nyimbo sita ambazo ni ‘Afrika Kilomondo’, ‘Afrika Yetu’, ‘Mama Mwenye Nyumba’, ‘Mwandani’, ‘Manzila’ na ‘Njoo Tu’. Wasanii ambao sauti zao zitasikika katika albamu hiyo ni Isack, Ali Choki, Luiza Mbutu, Bob Ludala, Keysha na Juma Nature.
Wednesday, March 18, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment