Wednesday, March 18, 2009

WATU WANGU NT ILIKUWA INASUMBUA BY THE TIME NAINGIZA HAYA MA-NEWS ILA MSIKONDE IKIWA FRESH NITAWEKA PICHA ZA KILA MSANII ANAYEHUSIKA...KWA CHOCHOTE KAMA KAWA NICHEKI KUPITIA haramba29@yahoo.co.uk

NAMELESS KUPIGA KOLABO NA BLUE 3



Blue 3 kutoka Uganda washindi wa Coca Cola Pop Star wanatarajia kushirikiana na Nameless kutoka Kenya kwenye wimbo wa Prisoner.

JUMANNE IDDY AKANA KUUZA GARI LA BSS

Tunda la kwanza la BSS Jumanne Idd amesema gari alilopata kama zaiwadi ya BSS bado animiliki na hana mpango wa kuifanya Tax “Gari huwa ninawapa washkaji zangu sometimes waka-spend so wabongo walipoona hivyo wakajua nimeiweka sokoni, gari ile ni kumbukumbu kubwa kwangu na kwa watoto wangu hapo baadaye” siad J4
Akilonga kupotea kwake kwenye anga za flava anadai bado yupo na anaandaa albam yake ya pili itakayaojulikana kwa jina la "Tawile" ikiwa na mawe kumi.

"Tawile ni shukrani kwa watu wangu walionisaidia kufika hapa nilipo, katika baadhi ya nyimbo ni "Popi", "Mnielezee", "Ole Wako", "Mapenzi Dhahabu", "Mapenzi Matamu".

HATARI LAKINI SALAMA!!!!

NYAMWELA KUFANYA KAZI NJE YA TWANGA

Mcheza show mkongwe wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Hassan Mohamed maarufu kwa jina la Super Nyamwela, amesema baada ya albamu yake ya kwanza aliyoitengeneza nje ya bendi yake kupata mafanikio katika soko la muziki. Anatarajia kuachia albamu yake ya pili ambayo mpaka sasa bado hajajua itaitwaje.

Akizungumzia habari hizo Nyamwela anasema amepanga mpaka kufikia mwezi Aprili mwaka huu awe amekamilisha albamu itakayokuwa na nyimbo sita na kuingia sokoni. “Master On The Temple” ndio jina la albamu yake ya kwanza. Nyamwela amedumu kwenye bendi ya Twanga Pepeta tangu mwaka 2000 akitokea kundi la Billi Bums lililokuwa likifanya show kwenye ukumbi wa Billicanas.

“Sijajua niipe jina gani mpaka sasa ila itakuwa na nyimbo sita ambazo ni ‘Afrika Kilomondo’, ‘Afrika Yetu’, ‘Mama Mwenye Nyumba’, ‘Mwandani’, ‘Manzila’ na ‘Njoo Tu’. Wasanii ambao sauti zao zitasikika katika albamu hiyo ni Isack, Ali Choki, Luiza Mbutu, Bob Ludala, Keysha na Juma Nature.

ZOLA D APATA TUZO NCHINI KENYA




Baada ya kuona muziki wa Bongo ukimzingua pasipo kupata mafanikio ya anavyotaka msanii wa kufoka foka wa kitanzania Zola D ameamua kuhamishia kazi zake nje ya mipaka ya Tanzania kwa kutafuta soko la nje na kwakuanzia anasema kuwa amepata tuzo kwenye tuzo zinazojulikana kwa jina la Coastal Music Awards (KE) kupitia wimbo wake wa "Hoi" aliyofanya pamoja na Cannibal wa Kenya.

"Bongo nimeona sifanikiwi kivile na ndio maana nimeona bora nielekeze nguvu zangu nje ambako nathaminiwa zaidi kuliko hapa nyumbani, mpaka sasa nimeshatengeneza kazi zaidi ya nane na Cannibal. Na katika kutanua wigo zaidi natarajia kufungua kituo changu cha radio katika nji wa Moshi. kwasasa nina safari ya kuelekeea bara la Ulaya kwanza kisha nikirudi ndio nakamilisha mambo yote yaliyobaki" alinena Zola D

Monday, March 9, 2009

MODOZ & JOHN WA MUZIKI MNENE




Hawa ni wana walikutana nami mtumzima wakatamani kuuza sura kwenye blog yangu bila hiyana tukajifotoa kisha nimewauzisha, washkaji waliniambia wanadili na umodo...anyway mimi ni huyo niliyevaa t-shirt ya njano yenye mishari.

KUTOKA KENYA MPAKA BONGO




Kwa jina anajulikana kama Wamboh aka Lonah ni demu anayetokea pande za Kenya akiwa ametua Bongo kwaajili ya kufanya mavituzi kwenye anga za Bongo Flava, so mabibi na mabwana kaeni tayari kumwona kimwana huyu na kumjua zaidi kupitia site yenu ya muziki mnene.

NO BEEF WITH CHAMELLIONE



Baada ya kuwa katika malumbano ya muda mrefu hatimaye wasanii nguli wa Uganda Jose Chamilleone na Bebe Cool wametangaza kutokuwa na beef baina yao, akizungumza na wanahabari Jose amesema sio kwamba walikuwa na beef bali kila mtu alikuwa bize katika imaya yake akitafuta soko la muziki lakini haimaanishi kuwa walikuwa nabeef kati yao. "Bebe ni rafikii yangu tangu kitambo na bado ataendelea kuwa rafiki yangu" alisema Chamellione

DAYNA KUTOA VIDEO NA MARLAW



Mwanadada Dayna kutoka pande za Moro hivi sasa yuko bize chini ya kampuni ya EMPTY SOUL akishoot video yake ya MAFUNGU aliyoshirikiana na Marlaw. kwa mujibu wa Dayna video hiyo itafanyika katika mikoa ya Moro na Dar na anaamini kitatoka kitu cha ukweli