Baada ya wasanii Nazizi, Wyre (Kenya) kuungana na Bebe Cool (Uganda) na kuunda kundi la E.A.B.C wasanii wengine Matovu Haruna 'Nash RiverNile, Ssent Sam 'Spire Man' (Uganda) kuungana na Wahyda Mohamed 'Y' (Tanzania) na kuunda kundi la Data Base.
Akizungumzia muungano huo mmoja kati ya wasanii wa kundi hilo Nash amesema kuwa wameamua kumwongeza mwanadada huyo katika kundi lao ili kuongeza ladha zaidi na kuwavuta watanzania ili waweze kuwaelewe kwakua kwa asilimia kubwa wao watatumia kiganda katika mashairi yao wakati ambapo mwanadada Y anatumia kiswahili zaidi.
Kwa sasa Nash anatamba na nyimbo zake za “Kuwa Na Wewe” na “Tugende Kampala” aliomshirikisha QJ ndio. Huku wakiwa kwenye maandalizi ya kutoa wimbo wao wa kundi wa 'Tuzine' unaotayarishwa na Hermy B.
KWENYE PICHA HUYO NDIYE NASH RIVER NILE
No comments:
Post a Comment