Wednesday, April 15, 2009

G-SOLO KUREKODI NA COMMON




Msanii wa Tanzania Gerald Mwanjoka ‘G-Solo’ aliyewahi kurekodi wimbo mmoja na msanii maarufu wa hip hop wa Marekani LL Cool J uliojulikana kwa jina la Hip Hop Is Everywhere. Inasemekana yupo kwenye mipango ya kurekodi na msanii mwingine wa Marekani anayejulikana kwa jina la Common. Ameshafanya mipango na ikikamilika G-Solo ataelekea Marekani kufanya kazi hiyo.

Akiongea na John Joseph wa muzikimnene mshkaji amekiri kuwa ni kweli mkakati huo upo na mambo yakiwa freshi atawajulisha wadau wote wa kile kinachoendelea.

No comments: