Wednesday, April 15, 2009

Nina weza kote, muziki na filamu




Baada ya kuonyesha kipaji kwenye uimbaji hivi sasa Isabela Mpanda ameamua kuhamishia majeshi kwenye uigizaji lakini akisisitiza kuwa hajaacha kufanya muziki.

Msanii huyu aliyetamba na nyimbo za Nimedata na Penzi Lateja ameshashiriki kwenye filamu mbili ikiwemo filamu ya Poja inayotarajiwa kutoka hivi karibuni. “Mimi ni msani wa ukweli naamini naweza nikahimili kazi zote kwakua ninakipaji cha ukweli. Wapenzi wangu wategee mambo mengi katika pande zote ninazoshiriki” alinena Isabela

Pichani ni ISABELA akiwa katika pozi alipokutana na John Joseph wa muzikimnene.blogspot.com

No comments: