Saturday, April 25, 2009

MWIZI WA KITI UWANJA WA TAIFA



Kamanda a pilisi kanda maalum ya kipolisi Dar es salaam akimwonyesha kwa waandishi wa habari kijana aliyekamatwa akiiba kiti katika uwanja wa taifa siku ya mpambano baina ya Simba na Yanga..

Duuuu mshkaji noma kweli halafu mbaya zaidi ni dent wa chuo flani hapa mjini,,ngoja nikiifadhi maana isije kuwa taaaabu

Wednesday, April 15, 2009

WABONGO NDANI YA ALGERIA!!!




HAWA NI WABONGO WALIO ALGERIA WAKIJIACHIA,,,JAMAA HAWAJAENDA KUUZA SURA TU ILA WAMEENDA KUKAMU BOOK.

MAJI MAJI MAJI MAJI



HAWA VIJANA WANAKOMAAA NA MAJI,,,DDUUUUUUUU AMA KWELI JIJI LA DAR MAJI TAAABU MPAKA WANAJUUUUUUUTA KUJA JIJINI!!!!

MAJINA YAO NI SIRI YANGU MAANA WAKIJUA KAMA NIMEWAWEKA KWENYE NET WATANIMALIZA

FULL KUJIACHIA NA UBWABWA!!!!!



MSHKAJI ANAKAMUA UBWABWA!!!! JAMAA ALIJITAMBULISHA KWA JINA LA CHUMU LAKINI UDAKU WANGU ULINIAMBIA KUWA JAMAA ANAJULIKANA KWA JINA LA SALIM NI MKAZI WA KIPAWA - KARAKATA

G-SOLO KUREKODI NA COMMON




Msanii wa Tanzania Gerald Mwanjoka ‘G-Solo’ aliyewahi kurekodi wimbo mmoja na msanii maarufu wa hip hop wa Marekani LL Cool J uliojulikana kwa jina la Hip Hop Is Everywhere. Inasemekana yupo kwenye mipango ya kurekodi na msanii mwingine wa Marekani anayejulikana kwa jina la Common. Ameshafanya mipango na ikikamilika G-Solo ataelekea Marekani kufanya kazi hiyo.

Akiongea na John Joseph wa muzikimnene mshkaji amekiri kuwa ni kweli mkakati huo upo na mambo yakiwa freshi atawajulisha wadau wote wa kile kinachoendelea.

Nina weza kote, muziki na filamu




Baada ya kuonyesha kipaji kwenye uimbaji hivi sasa Isabela Mpanda ameamua kuhamishia majeshi kwenye uigizaji lakini akisisitiza kuwa hajaacha kufanya muziki.

Msanii huyu aliyetamba na nyimbo za Nimedata na Penzi Lateja ameshashiriki kwenye filamu mbili ikiwemo filamu ya Poja inayotarajiwa kutoka hivi karibuni. “Mimi ni msani wa ukweli naamini naweza nikahimili kazi zote kwakua ninakipaji cha ukweli. Wapenzi wangu wategee mambo mengi katika pande zote ninazoshiriki” alinena Isabela

Pichani ni ISABELA akiwa katika pozi alipokutana na John Joseph wa muzikimnene.blogspot.com

Thursday, April 2, 2009

TANZANIA + UGANDA = DATA BASE



Baada ya wasanii Nazizi, Wyre (Kenya) kuungana na Bebe Cool (Uganda) na kuunda kundi la E.A.B.C wasanii wengine Matovu Haruna 'Nash RiverNile, Ssent Sam 'Spire Man' (Uganda) kuungana na Wahyda Mohamed 'Y' (Tanzania) na kuunda kundi la Data Base.

Akizungumzia muungano huo mmoja kati ya wasanii wa kundi hilo Nash amesema kuwa wameamua kumwongeza mwanadada huyo katika kundi lao ili kuongeza ladha zaidi na kuwavuta watanzania ili waweze kuwaelewe kwakua kwa asilimia kubwa wao watatumia kiganda katika mashairi yao wakati ambapo mwanadada Y anatumia kiswahili zaidi.

Kwa sasa Nash anatamba na nyimbo zake za “Kuwa Na Wewe” na “Tugende Kampala” aliomshirikisha QJ ndio. Huku wakiwa kwenye maandalizi ya kutoa wimbo wao wa kundi wa 'Tuzine' unaotayarishwa na Hermy B.

KWENYE PICHA HUYO NDIYE NASH RIVER NILE

MID MAN RECORDS VIPI



Hizi ni pande flani za Dar karibu na Rose Garden....Wazeyaaaa mnaikumbuka studio ya MID MAN RECORDS hawajamaa walitamba kipindi flani walipowatengenezea ngoma kundi la TMK NAJITA ile ngoma yao ya TWENDE na nyingine kadhaa lakini baada ya hapo wamepotea kusikojulikana. WAZEYAAA WIPI?????