Saturday, November 21, 2009

RATIBA YA WIKI YA BILICANS


Bilicanas Weekly Program

Wednesdays-
• Ngoma Afrika
• Entrance-5,000 tsh.
• Entertainment- Live Band, Dance Group

Thursdays-
• Ladies Paradise
• Entrance Ladies Free and Gents 5,000 tsh. With 5,000 drink coupon.
• Entertainment- Band + other entertainment.

Fridays-
• Zain Wonders Party
• Entrance 10,000 tsh
• Entertainment-Dancers and Dance Cages, Guest Djs/Competitions- Sexy Street Fashion Show- Extreme Pleasure All Night!!

Saturdays-
• Crazy Saturday Night Live with East Africa
• Entertainment-Live Video Mix- Dance Performance (MJ)-Dance Competitions and Mc Competitions + Dancers and cages. Pure Ecstasy!
• Entrance 10,000 tsh

Sunday-
• Way Back Sundays
• Live Band and Old School Sundays
• Entrance 5,000 tsh
• Entertainment-Live Band, Dj Music.

HAINA KUSHANGAA



Huyu jamaa kwao ndiyo HANDSOME

HII NDIO BONGOOOO!!!



Haina kushangaa, gari inaenda huku mlango unabaki nyuma....

MWANAMBOKA KUWAONGOZA WENZAKE JUMAPILI HII



Na John Joseph

TAMASHA maalum la watoto linalojulikana kwa jina la Red Ribbon Children's Day linatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kesho kutwa kwa kushirikisha wanamitindo kadhaa maarufu wa hapa nchini.

Katika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House (TMH) Khadija Mwanamboka ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, alisema wabunifu hao wameamua kushiriki ili kutoa burudani kwa watoto ili kuwaonyesha jinsi wanavyowajali. Pia alisema watakuwepo wasanii wa muziki wa kiazazi kipya watakaosindikiza shughuli hiyo.

Wanamuziki hao ni Marlaw, Hemed, Profesa Jay, Mo Racka, Matonya, Chid Benz na Quick Rocka ambao watataoa burudani kwa watoto na wengineo watakaofika siku hiyo kushuhudia.

Aidha alitaja wanamitindo wengine watakaokuwepo siku hiyo na kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki ni Mustafa Hassanali, Ally Remtullah, Franko, Zamda George, Farha Sulatan na Asia Idarous atakaecheza ngoma ya kizanzibari itwayo ‘Bomu’.

Pia kutakuwa na mashindano ya kuimba na kucheza na zawadi nyingi zitatolewa kwa watoto. Sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo ni Clouds FM, Channel TEN, Entertainment Masters, Profesa Jay Foundation, Tanzania House of Talent (THT), Mokasi Medical System, Cool Blue na Shear Illusion.


MWISHO

Friday, November 20, 2009

MPOKI WA ZE KOMEDI APATA AJALI NA KUVUNJIKA MKONO



Mpoki, mwigizaji maarufu wa kundi la Ze Original Komedy (kulia) amepata ajali ya gari usiku wa kuamkia jana, na inasemekana amevunjika mkono wake wa kushoto ambapo mfupa umeachia.
Habari kutoka ndani ya kundi hilo zinasema hali yake sio mbaya sana na jana aliruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali ya Kairuki iliyoko mikocheni jijini Dar, na ataendelea na matibabu akiwa nyumbani.
Ajali hiyo ilitokea mikocheni wakati gari alilokuwa anaendesha lilipogongana uso kwa uso na Rav4 iliyokuwa inaendeshwa na mwanamama ambaye naye kalazwa hospitali ya TMJ.

Sunday, November 15, 2009

JOHN JOSEPH HARAMBA NA WADAU TUKIJIACHIA



Hapa mtu mzima nilikuwa na washkaji na wafanyakazi wenzangu tukijiachia, ilikuwa ni furaha tupu ndani ya BILICANAS

SEVEN NA SALEH ALLY



SEVEN AKIYARUDI NA SALEH ALLY KWENYE WELCOME PARTY YA ELIZABETH WA BIG BROTHER KWENYE UKUMBI WA BILICANAS

HATA MIMI NIMO !!!



Hata mimi mdau wenu JOHN JOSEPH nilikuwepo na dada Lucy Kiwere...mnamkumbuka??

ELIZA IF U DO ME I DO U



MAMBO YALIKUWA SIO MCHEZO!! HAPA ELIZABETH ALIKUWA AKICHEZA HUKU AMEZYNGUKWA NA WADAU KIBAO...

ELIZABETH WA BIG BROTHER AKIYARUDI MANGOMA



\Mwakilishi wa TANZANIA katika shindano la Big Brother, Elizabeth Gupta akiwa anayarudi mangoma katika sherehe maalum ya kumkaribisha iliyofanyika kwenye ukumbiwa BILICANAS mwishoni mwa wiki hii... mambo yalikuwa sio mchezo

NAOMI NDANI YA BONGO.



Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Marekani Naomi Campbel akiwa ndani ya Bongo hivi karibuni.

JK AKIWA NA JD NA G. HABASH



Judith Wabura aka Lady Jay Dee akiwa pamoja na Jakaya Kikwete pamoja na mumewe Gadner G. Habash wakati wa hafla ya MO Ibrahimu iliyofanyika Dar es salaam mwishoni mwa wiki huu

RAIS WA FIFA vs RAIS WA NIGERIA



Rais wa FIFA, Joseph Sepp Blatter (kushoto) akikabidhi medali ya FIFA KWA Rais wa Nigeria , Umaru Yar'Adua mnamo Novemba 15, katika mji wa Abuja.

MWENDO WA MAUZO KWA KWENDA MBELE



Mshkaji wangu anayepiga mzigo katika kituo cha MLIMANI TV, akiwa kwenye pozi na kombe la Ligi Kuu ya England.

KOMBE LA BARCLAYS LIKIWA NA WABONGO



Kombe la ligi kuu ya soka ya England lilipotua Bongo, fans kibao walijitokeza kupokea Kama wanavyoonekana baadhi ya wadau wakipozi kwaajili ya picha.

HUZUNI UJERUMANI



Wachezaji wa soka wa Ujerumani wakibeba jeneza lenye mwili wa kiwa wa nchi hiyo aliyejiua wakati wa kuuaga mwili wake.

Thursday, November 12, 2009

ELIZABETH GUPTA AKIINGIA BONGO



Elizabeth alipokuwa kiikanyaga ardhi ya Bongo mara baada ya kuwasili Jumatano ya wiki hii.

ELIZABETH AKIWASILI BONGO



Mshiriki wa Tanzania aliyekuwepo kwenye jumba la Big Brother akiwasili kutoka Afrika Kusini alipokuwa akishiriki baada ya kutolewa kwenye kinyang'anyiro hicho wiki iliyopita. Hapa likuwa amemkumbatia mtoto wa mmoja kati ya ndugu zake wealiofika kumpokea uwanja wa ndege

Sunday, November 1, 2009

MB DOG YUPO NJIA PANDA



KUMEKUWA na taarifa kuwa MB Dog aliyejitoa katika kundi la Tip Top CONNECTION yupo njia panda kuhusu kurejea kundini au la kutokana na kuyumba katika kujisimamia kazi zake. Tangu alipotoka kundini mwaka jana hajatoa albamu nyingine tangu ile ya kwanza ya ‘Ratifa’ aliyokuwa chini ya Tip Top.

UNIQ MODOZZ KUPATIKANA BONGO



MMOJA kati ya wadau wa urembo nchini Taji Liundi ambaye anamiliki mtandao wa komputa wa modotz.blogspot.com, ameandaa shindano la kuwapata wanamitindo chipukizi mchakato utakaofanyika hivi karibuni na kujulikana kwa jina la Uniq Modo.

Akielezea mchakato huo alisema hawatozingatia kimo cha washiriki tofauti na dhana iliyopo kuwa mwanamitindo lazima awe mrefu. “Hata kwa wale ambao hawatabahatika kushinda, tutahakikisha inawajali kwa kuwatafutia kazi mbalimbali za uanamitindo kwa wale watakaoonyesha kuwa na nia ya kujiendeleza kwenye fani hiyo.” alisema

Alifafanua kuwa shindano la Uniq Modo ni mwanzo wa safari ndefu ambayo itafungua njia kwa vijana wengi wenye nia na vipaji vya fani hiyo kuweza kujitangaza kitaifa na kimataifa.



MWISHO