Nyomi la wanadini wakitoa waraka wao katika viwanja vya Mnazimmoja
Sunday, August 30, 2009
Sunday, August 2, 2009
MAPACHA WA HIP HOP WAJITOSA KWENYE MUVI

Wasanii wawili wa muziki wa Hip Hop nchini wanaojulikana kwa jina la ‘Mapacha’ Levison Kasulwa na James Kasulwa wameamua kujitosa katika uigizaji wa filamu kwa kile walichosema wanataka kujaribu maisha ya upande huo.
Mapacha waliotamba na nyimbo za ‘50 50’, ‘Jipe Moyo’ na ‘Sababu Ya Pesa’ wanatarajia kushiriki katika filamu inayojulikana kwa jina la ‘Sizya’ ambapo wao ndio waigizaji wakuu pamoja na mkongwe wa filamu nchini Lumele Matovolwa maarufu kwa jina la ‘Bigie’.
“Waandaaji wa filamu hiyo kampuni ya Chapakazi waliona tunafaa na wakaamua kutushirikisha katika filamu hiyo lakini haina maana tumeiweka kando iliyotupa umaarufu” alisema Levison
MAYA: BADO NIPO NIPO KWENYE FANI
Maya ni mmoja kati ya waigizaji aliyetamba mwanzoni mwa miaka ya 2000 katika michezo kadhaa ya televisheni iliyokuwa ikionyeshwa na kituo cha ITV ambayo iligizwa na kikundi cha Kaole Sanaa Group, amesema bado anaendeleza fani hiyo licha ya kutoonekana mara kwa mara katika vipindi hivyo.
“Nimeajiriwa kwenye kampuni ya Game 1st Quality inayojihusisha na masuala ya filamu, hivyo akili yangu yote ipo kwenye kuigiza filamu na sio maigizo ya kwenye televisheni.” Alifafanua Maya
Alisema ameamua kujibidiisha kwenye filamu kwakua zinalipa tofauti na maigizo ya kwenye televisheni, pia nia yake ni kujiendeleza kimataifa akidai Game 1st Quality wana malengo mazuri na wasanii wanaofanya nao kazi akimtolea mfano Kanumba kwa kusema kampuni hiyo imemsaidia kuonekana na kufika mbali.
ALLY CHOKI YUPO KENYA

Video za Extra Bongo kurekodiwa Kenya
Kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki yupo jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya kuandaa mazingira ya kurekodia video za nyimbo zao mpya.
Katika ziara hiyo Choki alisema yupo nchini humo kwaajili ya kuongea na kampuni itakayotumika kurekodi video hizo japo alisema ni mapema mno kutaja jina la kampuni hiyo na kuahidi ataweka wazi mara atakaporejea nchini.
Albamu ya Extra Bongo inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ikijulikana kwa jina la ‘Mjini Mipango’ ambao ni jina la moja ya wimbo unaopatikana ndani ya albamu hiyo ikiwa ni utunzi wa Choki mwenyewe.
NIMECHILL NA TWINS!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)